Mbunge CCM ahoji ahadi ya Rais Magufuli kule Mererani

Ni kuhusu vijana walioshiriki shughuli za ujenzi wa ukuta wa Mererani

Mbunge CCM ahoji ahadi ya Rais Magufuli kule Mererani

Ni kuhusu vijana walioshiriki shughuli za ujenzi wa ukuta wa Mererani

31 May 2018 Thursday 16:54
Mbunge CCM ahoji ahadi ya Rais Magufuli kule Mererani

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Chumbuni Ussi Pondeza (CCM) amehoji ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa huko Mererani mkoani Manyara wakati akizindua ukuta uliozungushiwa kwenye mgodi wa madini aina ya tanzanite.

Alisema kuwa alipokuwa huko Rais Magufuli aliagiza vijana 2500 wa JKT waliojenga ukuta huo waajiriwe na vyombo vya ulinzi na usalama na kutaka kujua hatua zilizofikiwa tokea agizo hilo.

Akijibu, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, alisema kuwa ni kweli Rais Magufuli alitoa agizo hilo ambalo tayari limeanza kutekelezwa.

Alisema kuwa zoezi hilo limeanza na jeshi la polisi ambapo tayari kibali cha ajira kimekwisha tolewa na usaili umeanza.

Alidokeza kuwa vyombo vingine vitaendelea na zoezi hilo mara baada ya kutolewa kwa kibali cha ajira kutoka serikalini.

Akifafanua alisema kuwa jeshi la kujenga taifa lina mashamba makubwa ambayo hutumiwa na vijana kwa ajili ya kujifunza ili wakimaliza waende kuanzisha shughuli zao.

Aliongeza kuwa mashamba ya JKT si kwa ajili ya kulima bali ni kutoa ujuzi na baadaye vijana hao wanaweza kuanzisha miradi yao.

Kwa mujibu wa Mwinyo vijana walioajiriwa na jeshi hilo kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2017 ni 42,593.

Kuhusu fidia kwa maeneo yaliyochukuliwa na jeshi, alisema kuwa fedha zitalipwa kwa wahusika kutokana na upatikanaji utakavyoruhusu.

Alidokeza kuwa mabilioni ya shilingi yamekwisha tengwa kwa ajili ya kulipa fidia ikiwemo wananchiwa jimbo la Tarime mjini, mkoani Mara.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.