Mbunge CCM aungana na wa Chadema kuichachafya serikali

Ni John Heche na Stanslaus Mabula

Mbunge CCM aungana na wa Chadema kuichachafya serikali

Ni John Heche na Stanslaus Mabula

14 June 2018 Thursday 13:09
Mbunge CCM aungana na wa Chadema kuichachafya serikali

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Bunge Andrew Chenge ameiagiza serikali kuja tena na majibu mengine kuhusu muongozo alioutoa Mbunge wa Tarime vijijiini (Chadema) John Heche na yule wa Nyamagana Stansalaus Mabula (CCM) kuhusiana na katazo la usafirishaji wa Carbon kwa ajili ya kusafishia dhahabu.

Akiongea muda mfupi leo baada ya maelezo ya waziri wa Madini, Angela Kairuki kuhusu kauli ya serikali kuhusiana na mwongozo huo, mwenyekiti huyo alisema kuwa mwongozo wake ni kuwa pamoja na maelezo mazuri ya serikali lakini pia kuna upande wa pili lazima usikilizwe.

Chenge alisema kuwa muda wa kupiga marufuku usafirishaji wa carbon kutoka eneo moja kwenda lingine ni mdogo.

Alisema kuwa kuna umuhimu wa kutoa fursa kwa upande wapili wa kusikiliza hoja zao.

Alisema kuwa ni kweli serikali inatakiwa kupata kodi zote stahiki. Lakini bila kuwaumiza wafanyabiashara hao.

Aliongeza kuwa madini ya dhahabu yanapatikana sehem nyini na kuna wawekezaji wengi na kuitaka serikali kuwapatia majibu baada ya pande hizo kukaa pamoja.

Aidha Chenge alisema kuwa anaimani serikali itakuja na majibu na haibabaishi na kuongeza kuwa anamuamini sana waziri husika.

Kwa upande wake Mbunge wa Nyamagana, (CCM) Stanslaus Mabula alisema katazo lililotolewa na wizara limeleta taabu kubwa sana kwa wafanyabiashara.

Alisema kuwa serikali inatakiwa isaidie tatizo hilo kwani inawezekana ni usimamizi duni wa mapato unaofanywa na watendaji.

Alisema kuwa kama usimamizi wa mapato Geita uliimarishwa na serikali ikapata mapato hakuona sababu kwa jambo hilo kufanyika katika maeneo mengine kwani rasilimali ya dhahabu ni wananchi wote.

Aliitaka serikali kutafakari upya katazo hilo kwani kuna wengine pia walichukua mikopo benki na hivyo kuweza kuleta athari kubwa ya dhamana walizoweka.

Akizungumza awali, Waziri Kairuki alisema kuwa katazo hilo lililenga katika kuzuia mianya ya ukwepaji wa kodi, utoroshaji wa madini uliokuwa unafanywa na wafanyabiashara wasiowaaminifu.

Alisema kuwa kutokana na kukua kwa teknolojia, kila mkoa unaweza ukawa na mtambo wa uchenjuaji wa dhahabu na hivyo kupunguza au kuondoa kabisa kero hiyo.

Alibainisha kuwa matukio mengi ya wizi wa carbon yaliripotiwa huko Geita ambapo serikali pia ilikosa kukusanya mapato yake yanayokadiriwa kufikia shilingi milioni 103.Matukio pia yaliripotiwa Mwanza na, Handeni

Alidokeza kuwa zoezi la usafirishaji wa carbon liligubikwa na utata mkubwa na kwa katazo hilo serikali iliongeza kiasi cha kodi.

Alisema kuwa serikali ya Rais John Magufuli ipo makini na kamwe haiwezi kukubali kuendelea kuona ukwepaji wa kodi kwenye sekta hiyo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.