banner68

Mbunge CCM kumpambanisha Naibu Waziri na wananchi kuhusu mradi wa maji usiopewa kipaumbele

Ni wa huko Mkomazi mkoani Tanga

Mbunge CCM kumpambanisha Naibu Waziri na wananchi kuhusu mradi wa maji usiopewa kipaumbele

Ni wa huko Mkomazi mkoani Tanga

18 June 2018 Monday 11:57
Mbunge CCM kumpambanisha Naibu Waziri na wananchi kuhusu mradi wa maji usiopewa kipaumbele

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Korogwe Mjini Mary Chatanda (CCM) amemtaka Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kutembelea mradi wa maji wa Mkomazi ambao serikali haijaupa kipaumbele

Chatanda alikuwa akiuliza swali la nyongeza bungeni leo ambapo alisema kuwa bado serikali haijaupa kipaumbele mradi huo na kumtaka Naibu Waziri huyo kwenda kuwaeleza wananchi wa Mkomazi.

Akijibu swali lake, Naibu Waziri Aweso alisema kuwa anatambua suala hilo lakini yeye yupo tayari kuongozana na Mbunge wa Jimbo husika Steven Ngonyani kutembelea mradi huo mara baada ka kikao cha bunge kumalizika.

Akijibu swali lingine lililoulizwa na Mbunge wa Mpwapwa George Lubeleje kuhusu skimu za maji kutofanyiwa matengenezo kwa miaka kumi alisema atautembelea.

Lubeleje alisema kuwa mji wa Mpwapwa na Kongwa kuna skimu za maji zilizojengwa zaidi ya miaka kumi iliyopita lakini hazijafanyiwa ukarabati.

Alisema kuwa hakuna mtaalam hata mmoja aliyezipitia na kumtaka Naibu Waziri huyo kueleza kama yupo tayari kwenda huko.

Akijibu Naibu Waziri Aweso alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa uchumi wa viwanda na umwagiliaji, atatembelea skimu hizo mara baada ya kikao cha bunge kumalizika.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.