Mbunge mstaafu Mteketa afariki dunia

Mbunge mstaafu Mteketa afariki dunia

19 June 2019 Wednesday 14:52
Mbunge mstaafu Mteketa afariki dunia
Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
MBUNGE mstaafu wa Kilombero, Abdul Rajabu Mteketa amefariki dunia.

Amefariki leo Juni 19, 2019 akiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) jijini Dar es salaam  akipatiwa matibabu.

Februari 11, 2018 Mteketa aliwahikuomba msaada wa kupatiwa matibabu ya upasuaji wa magoti yake.

Mbunge huyo aliyetumikia jimbo la Kilombero baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu mwaka 2010, alitumia njia ya video mtandaoni kupeleka ujumbe kwa Rais.

Februari 12, 2018  gari la wagonjwa lilifika na kumchukua kumpeleka Muhimbili. Kupitia Facebook video ya kwanza ilimuonesha  Mteketa akiomba msaada, ukafuatia ukurasa wa Facebook wa mkewe unaomshukuru Rais kwa msaada huku ukisisitiza kuwa wao wasingeweza. Video ya pili ilimuonesha mhusika akishukuru akiwa ndani ya gari la wagonjwa.
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.