Mchungaji na wake zake wahukumiwa kwenda jela

Mchungaji na wake zake wahukumiwa kwenda jela

10 September 2019 Tuesday 13:46
Mchungaji na wake zake wahukumiwa kwenda jela

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Septemba 10, 2019 imemuhukumu kwenda jela mwaka mmoja, Mchungaji Kanisa la The Hill Lord, David Chirhuza (33) na wake zake wawili kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Pia imemuhukumu mchungaji huyo mwenye wake watatu na watoto sita, kwenda jela mwaka mmoja kwa kufanya kazi ya uchungaji bila kibali cha makazi.

Hatua hiyo inafuatia baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani mchungaji na wake zake wawili na mdogo wake baada ya kukiri makosa ya kuingia nchini bila kibali akitokea nchini DRC Congo.

Pia kukiri kosa la kufanya kazi ya uchungaji bila kibali cha makazi

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Mmbando baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka yao na kukir

Mbali na mchungaji washtakiwa wengine ni wake wa mchungaji huyo Esther Sebuyange (27), Kendewa Ruth (26) na mdogo wa mchungaji, Samuel Samy (22).

Baada ya kusomewa mashtaka yao, Mchungaji David alikiri shtaka la kwanza la kuingia nchini bila kibali na kukiri shtaka la pili kufanya kazi ya uchungaji huku akiwa hana kibali cha makazi.

Washtakiwa wengine walikiri shtaka la kuingia nchini bila kibali

Washtakiwa hao kabla ya kuhukumiwa waliomba mahakama iwasamehe, isiwape adhabu kali, huku mchungaji akisema kazi aliyokuwa akiifanya ya kuhudumia jamii si biashara pia kusimamia sheria ya Mungu.

Mashtaka waliyosomewa ni kuwa Septemba 2, 2019 eneo la Salasala Kilimahewa wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, mchungaji huyo na wenzake walibainika kuingia nchini bila kibali.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa mchungaji huyo pekee alibainika kujihusisha na kazi za Kanisa bila kuwa kibali cha makazi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.