Meneja maabara ya madini, wenzake wafikishwa mahakamani

Meneja maabara ya madini, wenzake wafikishwa mahakamani

16 July 2019 Tuesday 04:31
Meneja maabara ya madini, wenzake  wafikishwa mahakamani

N mwandishi wetu, Dar es Salaam
MENEJA wa Maabara wa Tume ya Madini, Donald Njonjo(30) na wengine wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka manne ya uhujumu uchumi likiwemo la kuiba madini ya dhahabu yenye thamani ya milioni 507.

Njonjo na wenzake, wamefikishwa Mahakama  Julai 15, 2019 na kusomewa mashtaka yao mbele ya  Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina.

Mbali na Njonjo, washtakiwa wengine ni Gamba Muyemba (51) maarufu kama Emmanuel mkazi wa Tandika pamoja na Kashif Mohamed (41) mkazi wa Upanga, ambao kwa pamoja wanadaiwa kuiba madini hayo kwenye Tume ya Madini.

Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori amedai kuwa, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo, kati ya Novemba 30, 2017 na Juni 29, 2019 katika Ofisi ya Tume ya Madini iliyopo Masaki wilayani Kinondoni.

Updated: 16.07.2019 04:37
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.