Meneja wa maabara mbaroni kwa wizi dhahabu za serikali

Meneja wa maabara mbaroni kwa wizi dhahabu za serikali

11 July 2019 Thursday 14:37
Meneja wa maabara mbaroni kwa wizi dhahabu za serikali

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linamshikilia Dornald Joseph Njonjo (30) Meneja wa maabara wa tume ya madini kwa tuhuma za kuiba  dhahabu mali ya serikali kilogram 6.244 yenye thamani ya Tsh 507,347,000/= yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye Kasiki katika ofisi za wakala wa madini Masaki Jijini Dar es salaam.

Kamanda wa kanda hiyo Lazaro Mambosasa amesema Juni 29, 2019  Polisi walipata taarifa kutoka kwa ally Sadick (40) afisa madini Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kugundua kuibwa kwa madini hayo ya dhahabu.

"Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa hizo lilianza uchunguzi mara moja na kubaini kuwa madini hayo yaliibiwa na Dornald Joseph Njonjo na kuwa alianza kuiba tangu mwaka 2018 mwezi Desemba''

''Baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kuiba madini hayo kidogokidogo ambayo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye chumba katika jengo la ofisi za tume ya madini zilizopo Masaki.

''Mtuhumiwa alieleza kuwa madini hayo aliyauza katika duka la kuuzia vito vya dhahabu na kisha kuhifadhi madini bandia yenye uzito wa kilo 6.001 nyuma ya jengo la tume ya madini ili kuyapeleka katika chumba walichoiba madini hayo halisi ili kuyabadilisha'' amesema.

Madini hayo halisi ya dhahabu yalikamatwa mwaka 2017 huko maeneo ya Bandarini Zanzibar yakiwa yanasafirishwa kinyume cha sheria kisha kuitafishwa na serikali na kuhifadhiwa katika ofisi za tume ya madini.

Polisinakamilisha utaratibu wa kupeleka jalada kwa mwendesha mashtaka wa serikali ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam liimefanikiwa kukamata silaha moja aina ya bastola FATIN 13- TURKEY yenye namba T.0622010J00535 ikiwa na risasi tisa ndani ya Magazine huko maeneo ya Tangi-bovu  Mbezi.

Mnano tarehe 04/07/2019 majira ya saa nne na nusu usiku kikosi maalum cha kuzuia na kupambana na majambazi kilifanikiwa kumkamata Michael Nina Stellu (27) Mkazi wa Tangi bovu akiwa na silaha hiyo ambayo inasadikiwa kutumika katika matukio ya kihalifu maeneo mbalalimbali ya Jiji.

Katika mahojiano na Jeshi la Polisi mtuhumiwa anakiri kupewa silaha hiyo na mwenzake  ambaye hamfahamu kwa jina ila anamtambua kwa sura na jina moja la “Mama mdogo”.

Jitihada za kumtafuta mtuhumiwa huyo zinaendelea.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.