banner68
banner58

Mfuko mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF kuanza kazi Agosti Mosi

Mfuko mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF kuanza kazi Agosti Mosi

31 July 2018 Tuesday 17:19
Mfuko mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF kuanza kazi Agosti Mosi

Serikali imetangaza rasmi kuanza kutumika kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuanzia Agosti 1, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, ambapo amesema kuwa Serikali imekamilisha maandalizi yote muhimu ya utekelezaji wa Sheria ya PSSSF na imeridhika kwamba Mfuko huo unaweza kuanza kutekeleza majukumu yake.

“Napenda kutangaza rasmi kwamba, kwa mamlaka niliyonayo chini ya kifungu cha 1(1) cha Sheria ya PSSSF nimeteua tarehe 1 Agosti, 2018 kuwa ndiyo tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya PSSSF,” amesema Mhagama

Aidha, Mhagama amefafanua kuwa, kutokana na hatua hiyo wafanyakazi wote watakaoajiriwa katika sekta ya umma watasajiliwa katika Mfuko wa PSSSF na wale watakaoajiriwa katika sekta binafsi watasajiliwa katika Mfuko wa NSSF.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Wanachama wote ikiwa ni pamoja na wastaafu na warithi waliopo katika mifuko inayounganishwa watahamishiwa katika mfuko wa PSSSF na haki na stahili zao zitaendelea kutolewa na mfuko huo bila kuathiriwa kwa namna yeyote ile.

Updated: 31.07.2018 17:22
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Hassan Ibrahim 2018-07-31 18:28:28

Nataka ajira

Avatar
Malkiadi 2018-07-31 20:41:56

Mkulima

Avatar
Jlunilija@gmail 2018-08-16 17:03:26

kuna mambo mhim Sana mifuko ya hifadhi ilikuwa inasaidia kama kuwasomesha wanachama kuwakopesha fecha kwa ajili ya kujiendeleza sijuwi kwa sasa imewekwaje hilk

Avatar
happy fungo 2018-08-20 22:04:03

mimi nilikuwa ppf nami nimeamishiwa mfuko gani psssf mimi mstaafu toka shirika la umma

Avatar
TITO GODPHREY NSIMAMA 2018-09-01 22:58:40

Kwa sasa makato tako sawa kwa wore? Namaanisha 5% hata NSSF?

Avatar
helard 2018-09-09 20:08:37

Vp kuhusu mikopo kwa wanaojiendeleza na shule