Mfumuko wa bei waongezeka nchini

Mfumuko wa bei waongezeka nchini

09 July 2019 Tuesday 09:01
Mfumuko wa bei waongezeka nchini

Na mwandishi wetu, Dodoma
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetangaza kuwa mfumuko wa bei wa taifa kwa  mwezi Juni,2019 umeongezeka hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.5 kwa mwezi ulioishia Mei,2019. 

Hayo yamesema  Julai 8,2019 jijini Dodoma na mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Daniel Masolwa na kuwa hali hiyo inamaanisha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa  mwezi Juni ,2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya iliyokuwepo kwa mwezi ulioishia Mei,2019.

Masolwa amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei  kumechangiwa kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Mwezi Juni, 2019 zikilinganishwa na bei ya bidhaa za mwaka ulioishia mwezi Juni, 2018.

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa Mwezi Juni, 2019 ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 3.6%,unga wa ngano kwa asilimia 4.4%, mtama kwa asilimia 4.9%, samaki wabichi kwa asilimia 27.3%, dagaa kwa asilimia 16.5%, mafuta ya kupikia kwa asilimia 9.5%, maharagwe kwa asilimia 3.0%, mihogo kwa asilimia 16.6% na viazi mviringo kwa asilimia 18.8%.

Aidha, Masolwa ametaja baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa Mwezi Juni,2019 ni pamoja na dizeli kwa asilimia 11.4%, petrol kwa asilimia 4.9, gharama za kulala kwenye nyumba za wageni kwa asilimia 5.8% na vitabu vya shule kwa asilimia 2.4%.

Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2019 umeongezeka hadi asilimia 2.3 kutoka asilimia 2.2% kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2019.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo wa Takwimu za Uchumi amezungumzia mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia Mwezi Juni, 2019 ambapo nchini Uganda mfumuko wa bei umeongezeka kwa asilimia 3.4% kwa mwaka ulioishia Mwezi Juni, 2019 Kutoka asilimia 3.3% kwa mwaka ulioishia Mwezi Mei, 2019 na Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Mwezi Juni, 2019 umeongezeka hadi asilimia 5.70% kutoka asilimia 5.49 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2019. 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.