Mhadhiri wa chuo kizimbani kwa rushwa ya ngono

Mhadhiri wa chuo kizimbani kwa rushwa ya ngono

14 August 2019 Wednesday 15:43
Mhadhiri wa chuo kizimbani kwa rushwa ya ngono

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MHADHIRI wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji,(NIT), Samsoni Mahimbo (68), leo agosti 14, 2019 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake ili amfaulishe katika mitihani wa marudio.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 12, 2017 huko katika nyumba ya kulala wageni ya Camp David iliyoko Mlalakuwa Mwenge.

Imedaiwa siku ya tukio, mshtakiwa akiwa muajiriwa wa chuo hicho cha NIT kama Mhadhiri kwa muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka 2015/2016 wa somo la usimamizi wa barabara na usafirishaji (road transport management), lenye kodi namba 07101 alitumia mamlaka yake kutokana na nafasi yake chuoni hapo na kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi, Victoria Faustine ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho anayosomea mafunzo hayo ya road transport management.

Imedaiwa kuwa mshtakiwa aliomba rushwa hiyo kama sharti kwa mwanafunzi huyo kuwa atamfaulisha katika mtihani wa marudio (Supplement) wa somo hilo uliokuwa ukifanyika Januari 5, 2017.

Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya milioni 4.

Upelelezi wa kesi hiyo umekamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 17,2019 mshtakiwa atakaposomewa maelezo ya awali.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.