Miili wafanyakazi Azam Media kuagwa leo Dar es Salaam

Miili wafanyakazi Azam Media kuagwa leo Dar es Salaam

09 July 2019 Tuesday 06:36
Miili wafanyakazi Azam Media kuagwa leo Dar es Salaam

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
MIILI mitano ya wafanyakazi wa Azam Media inatarajiwa kuagwa leo Julai 8, 2019 jijini Dar es Salaam.

Miili hiyo iliwasili jana usiku majira ya saa tano usiku kwa njia ya ndege na imehifadhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Mtangazaji wa Azam Tv, Baruani Muuza ameiambia Azanipost kuwa miili hiyo itaagwa leo katika ofisi za makao makuu ya Azam Media, Tabata T.O.T kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.

Amesema baada ya kuagwa watazikwa Dar es salaam, mwingine mkoani Kagera na Tanga.

Wafanyakazi wa Azam TV waliofariki kwenye ajali hiyo ni Salim Mhando (muongozaji wa matangazo), Florence Ndibalema (Mhandisi wa Sauti), Sylvanus Kasongo (Mhandisi Mitambo) na wapiga picha wawili Said Haji na Charles Wandwi.

Watu wengine wawili waliofariki ni dereva wa gari ambalo Azam TV walilikodi pamoja na msaidizi wake, majina ya wawili hao bado hayajapatikana. Wafanyakazi watatu wa Azam TV waliojeruhiwa ni Artus Masawe, Mohammed Mwinshehe na Mohammed Mainde.

Ajali hiyo  ilitokea majira ya saa 2:30 asubuhi katika  eneo la Kizonzo katikati ya  Igunga(Taboro) na Shelui (Singida)  ambapo  basi  aina ya  Coaster lililowabeba  wafanyakazi  wa  Azam  Media  Limited  likielekea  Mwanza limegongana uso kwa na uso na Lori la  mizigo  lililokuwa   Iinakwenda   Dar es Salaam.


Wafanyakazi wa Azam Media limited walikuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea kwenye sherehe za uzinduzi wa hifadhi va Taifa va Burigi-Chato kwa ajili va kurusha matangazo ya moja kwa moja ya sherehe hizo.

Updated: 09.07.2019 13:41
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.