Mke amuua mumewe kwa bisibisi

Mke amuua mumewe kwa bisibisi

05 August 2019 Monday 15:22
Mke amuua mumewe kwa bisibisi

Na mwandishi wetu, Pwani
MWANAMKE Mwajuma Omary Malembeka (28) anatuhumiwa kumuua mume wake Selemani Kondo (43) mkulima na mkazi wa Chamalale, kata ya Vihingo Mzenga, Wilayani Kisarawe mkoani Pwani kwa kumchoma na bisibisi kwenye bega.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Wankyo Nyigesa amesema mwanamke huyo alifanya maamuzi hayo kutokana na wivu wa kimapenzi.

"Kulikuwa na mzozo baina yao na Mwajuma alimtuhumu mume wake kuwa siyo mwaminifu katika ndoa yao. Selemani aliuawa kwa kuchomwa bisibisi katika bega  la kushoto na sehemu ya juu na mke wake huyo,”amesema kamanda Wankyo. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
 
Katika hatua nyingine, katika kijiji cha Lulenga Ubena, wilayani Chalinze Polisi wamemkamata Kitenye Lumange mfugaji wa jamii ya kimasai (24) kwa kosa la wizi wa ng’ombe 13 wenye thamani ya milioni 7.2 mali ya Arisen Hussein mkazi wa kijiji cha Visakazi . Kamanda huyo amesema wanawasaka watuhumiwa wengine walioshiriki kuiba mifugo hiyo.

Updated: 05.08.2019 15:30
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.