Mkuchika: Mkurugenzi wa Halmashauri anaweza kuitwa wakati wowote kuelezea Ilani ya CCM

Asema anaweza kujihusisha kwa kuwa ni wazi atakuwa na chama anachokipenda

Mkuchika: Mkurugenzi wa Halmashauri anaweza kuitwa wakati wowote kuelezea Ilani ya CCM

Asema anaweza kujihusisha kwa kuwa ni wazi atakuwa na chama anachokipenda

08 June 2018 Friday 12:27
Mkuchika: Mkurugenzi wa Halmashauri anaweza kuitwa wakati wowote kuelezea Ilani ya CCM

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Viti Maalum Ruth Mollel (Chadema) ameitaka serikali kueleza kama ipo tayari kuwaondoa kazini wakurugenzi wa halmashauri ambao bado wanajihusisha na siasa na wengine kuhudhuria vikao vya chama.

Alikuwa akiuliza swali la nyongeza bungeni leo ambapo alitoa mfano mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kuwa anahudhuria vikao cha chama cha mapinduzi (CCM) kinyume na sheria za utumishi wa umma.

Mbali ya watumishi Mollel ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu Mstaafu pia alisema kuwa kuna baadhi ya wakuu wa mikoa ambao wamekuwa wakiwa ni wakereketwa wakubwa siasa badala ya kufanya kazi za umma.

Akijibu, Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika alisema kuwa kwa mujibu wa kanuni 65(1) watumishi wa Umma hawatakiwa kujihusisha na mrengo wa kisiasa bali kuwatumikia wananchi bila ubaguzi.

Alisema kuwa kwa mujibu wa waraka wa utumishi wa umma namba 1 watumishi wa umma waliogombea na kupata uongozi walistafu na hawapo tena kazini.

Kuhusu wakurugenzi kujihusisha na siasa, alisema ni wazi kuwa atakuwa na chama anachokipenda.

Alidokeza kuwa Yule wa Ubungo kuhudhuria vikao vya CCM anafanya vile kuihoji serikali na pia anaweza kuitwa saa yoyote kuelezea utekelezaji wa Ilani cha chama cha mapinduzi.

Aliongeza kuwa Wakuu wa Mikoa ni wawakilishi wa Rais mkoani, na kamwe hawawezi kufanya mambo tofauti na kiongozi wa nchi.

Hata hivyo alisema kuwa endapo mtu yeyote hajaridhika na utendaji wa kazi wa wakurugenzi au wakuu wa mikoa basi anayo nafasi ya kwenda kupata tafsiri kwenye vyombo vya sheria kama Mahakama.

Azania Post

Updated: 08.06.2018 12:58
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.