Mkulima aliyefungua kesi kupinga ukomo wa urais aitwa mahakamani

Mkulima aliyefungua kesi kupinga ukomo wa urais aitwa mahakamani

02 October 2019 Wednesday 14:25
Mkulima aliyefungua kesi kupinga ukomo wa urais aitwa mahakamani

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imemtaka Dezydelius Patrick Mgoya ‘Mkulima’ aliyefungua kesi ya kikatiba kuhusu ukomo wa urais kufika mahakamani Oktoba 10, 2019 kufuatia maombi ya Chama cha ACT Wazalendo kujiunga na kesi hiyo.

Kesi hiyo (Misc Civil Cause No. 19 of 2019) ipo chini ya Jaji Dk Benhaj Masoud

Maombi ya ACT Wazalendo (Misc Civil Application No. 39 of 2019) kujiunga na kesi hiyo yameshindwa kusikilizwa leo kutokana na Dezydelius kutokuwepo Mahakamani.

Mahakama imeitaka ACT Wazalendo kutangaza wito wa kumuita mahakamani kwenye magazeti mawili yanayosomwa na wengi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama kimeomba kujiunga na kesi hiyo ili kuilinda na kuitetea Katiba.

Zitto amesema licha ya katiba ya sasa kuwa na mapungufu yake, inapaswa kuheshimiwa ikiwemo uwepo wa ukomo wa urais.

Katika hatua nyingine, Zitto amesema ACT Wazalendo imesikitishwa na uteuzi wa Dk. Wilson Mahera kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) huku ikifahamika wazi kuwa ni kada wa Chama cha Mapinduzi(CCM).

"Tumeshangazwa sana na hatua ya Rais Magufuli kuteua Mkurugenzi mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambaye rekodi zinaonesha amewahi kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM. Jambo hilo la wasimamizi wa uchaguzi ambao wana vyama vya siasa lipo mahakamani. Kwenye kesi ya Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe Mahakama Kuu ilisema wasimamizi wa uchaguzi hawapaswi kuwa wanachama, makada au mashabiki wa chama cha siasa. Tumesikitishwa na hatua ya Rais Magufuli kumteua mtu ambaye amekatazwa kuwa msimamizi wa jimbo moja na kumteua kuwa msimamizi wa nchi nzima," amesema Zitto.

Amesema kufuatia hali hiyo ACT Wazalendo inashauriana na vyama vingine vya upinzani kuhusu hatua za kisheria za kuchukua na tayari kimemuagiza Wakili Jebra Kambole atazame misingi ya kisheria ili kuzuia uteuzi huo wa Mkurugenzi mpya wa NEC.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.