Msaidizi wa Membe aliyetekwa, apatikana akiwa hai

Msaidizi wa Membe aliyetekwa, apatikana akiwa hai

10 July 2019 Wednesday 04:22
Msaidizi wa Membe aliyetekwa, apatikana akiwa hai

Na mwandishi wetu, dar es Salaam

ALLAN Kiluvya ambaye alidaiwa kutekwa na ni msaidizi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, amepatika akiwa hai.

Alitekwa na watu wasiojulikana  usiku wa kuamkia Julai 7, 2019 Jongoo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam na alipatikana majira ya saa tisa usiku Julai 8, 2019

Akizungumza  jana Julai 9, 2019, Allan amesema “Ni kweli mimi ni Msaidizi wa Membe na kuhusu watekaji walikuwa wanataka nini kwa kweli hilo siwezi kusema kwa kuwa tayari nimetoa maelezo Polisi na wao ndiyo watatoa hizo taarifa” 

“Walivyoniachia waliniuliza sehemu ipi itakuwa salama kwangu, nikawauliza kwanza hapa nilipo wapi wakaniambia ni Gongolamboto, nikawaeleza mimi nakaa Tabata Kinyerezi niacheni sehemu nitakayoweza kufika salama nyumbani”

“Nimeshatoa maelezo yangu kituo cha Polisi Kawe na wao wataeleza ukweli wote wa tukio na wasiposema, kwa kuwa mimi ni mpenda ukweli nitaeleza ukweli wote”

“Naamini Polisi watatoa ripoti kwa kile nilichoandika, naamini hawatotoka nje ya kile” Msaidizi wa Membe, Allan Kiluvya

“Naamini nitaendelea kuwa Msaidizi wa Membe” Alisisitiza  Allan Kiluvya

Updated: 10.07.2019 06:00
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.