Mtoto wa dereva wa RC aliyepata ajali afariki

Mtoto wa dereva wa RC aliyepata ajali afariki

06 August 2019 Tuesday 09:13
Mtoto wa dereva wa RC aliyepata ajali afariki

Na mwandishi wetu, Mara
MTOTO wa dereva wa mkuu wa mkoa wa Mara, Kasobi Shida(26) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Agosti 6, 2019 katika hospitali  ya mkoa huo.

Mtoto huyo alipata majeraha na kulazwa katika hospitali hiyo Agosti 4. Pia baba yake Shida Masabo(55) bado amelazwa hospitali hapo baada ya kuanguka kwa presha alipofika eneo ambapo mtoto wake alipopatia ajali wakati akiendesha gari ya Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima.

Kifo hicho kimethibitishwa na kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Mara, Dk Hosea Bisanda.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki amesema dereva huyo akipona atachukuliwa hatua kwa uzembe wa kuacha gari hadi ikachukuliwa na mwanae na kwamba kuna uwezekano huwa anamwachia kila mara.

Amesema mtoto huyo alichukua gari hilo baada ya baba yake kuiacha nje ikiwa inaunguruma kutokana na kupata mgeni wakati alipokuwa akijiandaa kulirudisha ofisini kwa mkuu wa mkoa alipomaliza kuliosha.

Alipofika katika eneo la Kwangwa, Musoma gari ilimshinda mtoto huyo kisha ikatoka nje ya barabara na kugonga ukuta wa daraja.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.