Mtuhumiwa mauaji mwanafunzi chuo kikuu akamatwa

Mtuhumiwa mauaji mwanafunzi chuo kikuu akamatwa

19 June 2019 Wednesday 13:58
Mtuhumiwa mauaji mwanafunzi chuo kikuu akamatwa
Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata Ernest Joseph (19) kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Mgaya aliyefariki dunia Juni 17 baada ya kuchomwa kisu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Juni 19, Kamanda wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa usiku wa kuamkia leo maeneo ya Madale jijini hapa.

“Mtuhumiwa katika mahojiano na Jeshi la Polisi amekiri kumchoma kisu kilichosababisha  kifo cha mwanafunzi huyo huku akieleza namna mwanafunzi huyo alivyokuwa amevaa siku hiyo ya tukio kuwa ni TSHIRT nyeusi,suruali ya Jinsi na Kapelo nyeusi.

“Aidha mtuhumiwa alikiri kumpora pochi iliyokuwa na simu moja aina ya Tecno rangi nyeusi,  fedha taslimu Sh 8,000 na vitambulisho mbalimbali ambavyo alivitupa na simu hiyo kuiuza,”amesema.

Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Usiku wa Juni 16, 2019 Anifa ambaye alikuwa anasomea Stashahada ya Maabara alishambuliwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana.

Anifa alikutwa na umauti majira ya saa 2 usiku jirani na geti la kuingia katika chuo hicho kilichopo Gongo la Mboto jijini Dar es Dar es Salaam alichokuwa akisoma.

Taarifa zilieleza baada ya kushambuliwa, wanafunzi wenzake walijitokeza ili kumpatia msaada kwa kumkimbiza hospitali lakini hadi wanafika alikuwa tayari umauti umemfika.
Updated: 19.06.2019 15:10
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.