Mwalimu mbaroni kwa kumpa ujauzito mwanafunzi

Mwalimu mbaroni kwa kumpa ujauzito mwanafunzi

05 August 2019 Monday 14:22
Mwalimu mbaroni kwa kumpa ujauzito mwanafunzi

Na mwandishi wetu, Manyara
JESHI la Polisi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara linamshikilia Mwalimu Daniel Saulo wa Shule ya Msingi Matui kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wake wa darasa la saba

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Christopher Foime amesema mtuhumiwa yupo kituo cha polisi Matui kwa ajili ya upelelezi na uchunguzi zaidi

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Victoria Mushi, alikiri kukamatwa kwa mwalimu huyo akisema tukio hilo ni la tatu kujitokeza shuleni hapo na kwamba hawezi kusema lolote kwa sasa

Baba mzazi wa mtoto huyo, Isaka Maro alieleza masikitiko yake kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Victoria Mushi kwa kuficha tukio hilo ingawa alilifahamu toka mwanzo baada ya shule kuwapima wanafunzi hao.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.