Mwinyi atoa neno picha na January Makamba

Mwinyi atoa neno picha na January Makamba

23 July 2019 Tuesday 06:37
Mwinyi atoa neno picha na January Makamba

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
Mzee Ali Hassan Mwinyi amezungumza kwa mara ya kwanza tangu January Makamba kuvuliwa uwaziri katika mageuzi aliyoyaidhinisha rais John Magufuli mwishoni mwa Juma.

Katika mahojiano namoja ya gazeti nchini, Mzee Mwinyi amesema, hakupenda 'kuona picha namna ile katika mazingira hayo'.

Amefafanua kwamba picha ile ni kama za kawaida wanazopiga watu wengi wanaokwenda kumuona na kuomba kupata ukumbusho.

'Lakini picha katika hali hii, alafu munang'onezana, munang'onezana nini? Sikuipenda' ameeleza Mzee Mwinyi.

January Makamba, aliyehudumu katika nafasi ya waziri wa Mazingira na Muungano nchini Tanzania alivuliwa wadhifa huo Julai 21, 2019 na nafasi yake kuchukuliwa na George Simbachawene.

Punde baada ya kutangazwa kutenguliwa kwake, Makamba aliweka picha yake akiwa amekaa na Mzee Mwinyi katika mtandao wa Twitter iliyoambatana na ujumbe:

"Ni kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa. Nitasema zaidi siku zijazo." Huku akiambatanisha maneno hayo na picha yake na rais msaafu Ally Hassan Mwinyi wakiwa wanaangua kicheko.

Mwanasiasa huyo mkongwe Tanzania aliye wahi kuhudumu pia kama rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania amesema hakustajaabishwa na picha hiyo ila amestaajabu wakati ambao picha hiyo imetolewa, 'kwanini ikawa sasa?'

'Kijana yule kaandika kitabu kaniomba niandike dibaji. Yumkini katika (occassion) hiyo, kuniomba au kunishukuru kufanya hivyo.'

Sikupenda mazingira, lakini silaumu wala sioni vibaya. Ila kwanini ikawe katika mazingira katika maji yaliokorogeka tuonekane tunanong'onezana. Tunanong'onezana nini? ameuliza Mzee Mwinyi.

'Ile picha ya zamani. Kwanini ikawa ndio sasa hivi ..., sasa hilo ndilo kidogo sikulipenda, limenishutua'.

Miongoni mwa aliyosifika nayo Makamba katika uongozi wake ni kufanikiwa kuidhinisha marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Hatahivyo akizungumza  mara baada ya kuapishwa kwa George Simbachawene, waziri mpya amechukua nafasi ya Makamba katika wizara ya mazingira na Muungano, Rais Magufuli amesema katazo hilo lilicheleweshwa.

"Nakumbuka kwenye suala la plastiki lilichukua muda mrefu, mpaka miaka minne. Nikasaini halikutekelezwa, Makamu wa Rais akazungumza, halikutekelezwa, Waziri Mkuu akaenda kuzungumza bungeni halikutekelezwa.

Mpaka hapa mwishoni nilipotoa amri ya lazima, ndipo likaanza kutekelezwa," ameeleza Rais Magufuli.

Kwa kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (Environmental Management Act) serikali ya Tanzania imetunga kanuni za mwaka 2019 za kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo ya plastiki.

Kifungu cha nane cha kanuni hizo kinaorodhesha makosa matano ambayo ni; kuzalisha na kuagiza mifuko ya plastiki, kusafirisha nje ya nchi mifuko ya plastiki, kuhifadhi na kusambaza mifuko ya plastiki, kuuza mifuko ya plastiki na mwisho kumiliki na kutumia mifuko ya plastiki.

Updated: 23.07.2019 06:45
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.