Nchi tisa zanunua vitunguu saumu nchini

Nchi tisa zanunua vitunguu saumu nchini

11 September 2019 Wednesday 12:30
Nchi tisa zanunua vitunguu saumu nchini

Na mwandishi wetu, Dodoma

SERIKALI imesema kwa sasa vitunguu saumu vimepata soko katika nchi tisa tofauti Duniani.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 11, 2019 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba na kwamba vinauzwa vikiwa mali ghafi.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay (CCM) aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kutafuta soko la vitunguu saumu nje ya Tanzania.

"Vitunguu saumu vinauzwa katika nchi ya Shelisheli, Visiwa vya Comoro, Msumbiji, Zambia, Mauritania, Kenya, Uganda na Falme za Kiarabu," amesema.

Mgumba amesema katika kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa mazao ya kilimo vikiwemo vitunguu swaumu, serikali imekamilisha upatikanaji wa simbomilia (barcode)pamoja na kubainisha viwango vya ubora kwa kulitumia Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Aidha, amesema wizara imeanzisha kitengo cha masoko chenye jukumu la kutafuta masoko ndani na nje ya nchi ikiwemo vitunguu saumu.

Hayo yote yanafanyika ili kuwa na taarifa sahihi za kuwapa wakulima waweze kuzalisha mazao yanayokidhi mahitaji ya soko.

Amesema, serikali kupitia Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) imevijengea uwezo vikundi vya wakulima katika bonde la Bashay na kuviwezesha kusindika vitunguu saumu.

‘‘Jitihada hizi zimesaidia kuongeza thamani ya zao la vitunguu saumu, muda wa kuvihifadhi bila kuharibika na kuimarisha soko la bidhaa hiyo ndani na nje ya nchi," amesema naibu waziri huyo.

Updated: 11.09.2019 15:27
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.