banner68
banner58

Ndugai kuingizwa kwenye kitabu cha maajabu ya dunia, baada ya kitendo cha leo bungeni

Ndugai kuingizwa kwenye kitabu cha maajabu ya dunia, baada ya kitendo cha leo bungeni

25 May 2018 Friday 11:17
Ndugai kuingizwa kwenye kitabu cha maajabu ya dunia, baada ya kitendo cha leo bungeni

Na Mwandishi Wetu

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai anaweza kuwa spika wa kwanza kuingia kwenye kitabu cha maajabu ya dunia (Guiness book of wonders) kwa kitendo chake cha kuonekana na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma ndani ya ukumbi wa bunge wakiwa pamoja wakati kikao kinaendelea.

Ilimbidi Mwenyekiti wa kikao cha bunge cha leo Ijumaa Musa Zungu kusitisha kwa dakika kadhaa kipindi cha maswali na majibu na kutangaza tukio hilo ambalo ni nadra sana kuonekana kwenye mabunge duniani.

Zungu alisimama na kusema kuwa kuna tukio muhimu ndani ya bunge la Tanzania na mengine ulimwenguni kote kwa jaji Mkuu na Spika aliyepo madarakani kukaa pamoja wakati bunge linaendelea na vikao vyake.

Wakati akisema hayo spika huyo na mgeni wake walisimama eneo la wageni wa spika na kupunga mikono huku wabunge wakishangilia kwa ndelemo na vifijo vingi.

Zungu alisema kuwa anaamini watu wa kamera wamelichukua tukio lile kwa uzuri na kuufahamisha ulimwengu.

Azania Post

Updated: 25.05.2018 19:17
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.