Paul Makonda awachongea Kubenea, Mnyika, Mdee kwa Rais Magufuli

Paul Makonda awachongea Kubenea, Mnyika, Mdee kwa Rais Magufuli

27 September 2018 Thursday 16:04
Paul Makonda awachongea Kubenea, Mnyika, Mdee kwa Rais Magufuli

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amelitumia Jukwaa la Uzinduzi wa Daraja la Juu (Mfugale Flyover) kuwamueleza Rais John Magufuli kuwa Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, Saed Kubenea wa Ubungo na John Mnyika wa Kibamba hawaungi mkono juhudi zake.

Uzindizu huo uliofanyika leo tarehe 27 Septemba, 2018 ambapo Makonda alitambulisha uwepo wa viongozi mbalimbali akiwamo Mbunge wa Temeke CUF Abdallah Mtolea na wengine wa Chama cha Mapinduzi CCM na kwamba alimueleza Rais kuwa wamefika wabunge na viongozi wa kada zote isipokuwa wabunge hao wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Makonda amepata kigugumizi kueleza alichokusudia baada ya kumueleza Rais kuwa wanasiasa hao hakuwakuwepo katika hafla hiyo ya uzinduzi.

”Mheshimiwa Rais ukiona yule wa Kawe hajaja, yule wa ubungo hajaja, Kibamba hajaja lakini aaah ….,” amesema Makonda bila kutoa maelezo kama walialikwa au la.

Amemtaja Mwita Waitara Mbunge wa Ukonga (CCM) kuwa yeye ndiye ishara ya kuwa CCM imekubalika kwa wananchi kutokana na ushindi wake wa asilimia 80.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo wa daraja hilo la juu linalounganisha barabara ya Nyerere na Mandela, Makonda amesema kuwa daraja hilo litapunguza changamoto ya foleni.

Makonda amemuomba Rais Magufuli kufanya ziara katika mkoa wa Dar es Salaam kwani wamekuwa wakiona wivu sana kuona wenzao wa mikoani wanavyopata nafasi ya kuonana naye.

Amesema kwa sasa juhudi za Rais Magufuli zimewafanya WanaCCM kutembea kifua mbele tofauti na ilivyokuwa zamani kwani hapo awali waliokuwa tukivaa nguo zao walikuwa wakizomewa lakini sasa hivi wanavaa kwa kujivunia.

Wakati huo huo ameeleza mikakati yake ya kuwawezesha walemavu kupata ajira. “Tumeamua kujipanga kimkakati kuitekeza sheria inayotoa haki na usawa kwa Ulemavu. Tumejipanga ili kila muajili ajili watu waremavu” Amesema Makonda.

Updated: 27.09.2018 16:13
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.