Polisi Mtwara wadhibiti wizi

Polisi Mtwara wadhibiti wizi

08 June 2018 Friday 11:16
Polisi Mtwara wadhibiti wizi

Na Mwandishi wetu

JESHI la Polisi mkoani Mtwara linawashikilia watu 15 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya wizi wa pikipiki na kutoa hundi hewa yenye thamani ya Tsh 9,450,000.

Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani humo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amesema kati ya May 27 na June 5, 2018 katika operesheni ya kukamata wahalifu mkoani humo, Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata pikipiki 7 za wizi aina mbalimbali pamoja na watuhumiwa 11 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.


RPC Mkondya ameongeza kuwa, watuhumiwa wanne kati yao na pikipiki mbili wamekamatwa katika Wilaya ya Tandahimba katika kijiji cha Maundo wakati watuhumiwa saba na pikipiki tano wamekamatwa katika Wilaya ya Mtwara Vijijini katika vijiji vya Mpapura, Kitere, Namgogori, Mabatini-Mpapura na Utendea ambapo watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Aidha, katika tukio lingine, RPC Mkondya amesema Jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kutoa hundi hewa yenye thamani ya Tsh 9,450,000 kwa lengo la kununua lita 4,000 za mafuta ya Petrol katika kituo cha Mafuta Ufukoni.

Upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea na watuhumiwa watafikishwa Mahakamani pindi utakapokamilika.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.