Polisi wa usalama barabarani wachangia foleni jijini Dar - wananchi

Ni wananchi waliozungumza na Azania Post

Polisi wa usalama barabarani wachangia foleni jijini Dar - wananchi

Ni wananchi waliozungumza na Azania Post

29 May 2018 Tuesday 09:32
Polisi wa usalama barabarani wachangia foleni jijini Dar - wananchi

Na Mwandishi Wetu

TATIZO kubwa la foleni kwa jiji la Dar es Salaam linasababishwa na matumizi ya binadamu kuongoza magari badala ya taa zilizowekwa.

Wakizungumza na Azania Post, baadhi ya abiria waliokuwa wanasafiri kwenye daladala namba T 356 CLI inayofanya safari zake kati ya Kawe na Mbagala walitaka jeshi la polisi kutotumia askari wake kuongoza magari kwenye mataa.

Walisema kuwa askari watumike kuongoza magari pale tu kunapokuwa hakuna umeme au kuna msafara wa viongozi tu.

Kwa mujibu wa abiria hao, askari akiwepo kwenye mataa hufanya upendeleo wa upande mmoja na kuwaacha wengine wakisubiri hata kwa zaidi ya saa nzima.

Wakitolea mfano, walisema kuwa kwenye makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Mwai Kibaki eneo la Moroko kunakuwepo na foleni zinazosababishwa na askari wa usalama barabarani hasa wakati wa jioni na asubuhi.

“Maajabu ni kwamba askari wanaongoza magari wakati taa zinafanya kazi matokeo yake ni kuwachelewesha wasafiri kule wanakokwenda,” alinasema mmoja wa abiria hao.

Kutokana na makadirio yaliyofanywa na DART mwaka 2010, Dar inapoteza bilioni 4 kwa siku kama gharama za mafuta yanoyapotea bure katika foleni, kupungua kwa ufanisi wa kazi na shughuli nyingine zinazoathirika kutoka na foleni jijini.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu unaonyesha kuwa, maeneo yenye foleni kubwa nyakati za asubuhi na jioni ni katika makutano ya barabara ya Kilwa na bandari, Nyerere na Msimbazi, Nyerere na Kawawa, Nyerere na Mandela, Kigogo na Morocco.

Azania Post

Updated: 29.05.2018 09:44
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.