Polisi wakamata majambazi saba

Polisi wakamata majambazi saba

11 July 2019 Thursday 14:07
Polisi wakamata majambazi saba

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watu saba kwa tuhuma za wizi wa bajaji maeneo ya Ukonga wilayani Ilala jijini  Dar es Salaam. 

Watuhumiwa hao ni Said Salum (27), Amo Kefas (30), Said Ahmad (38), Mohamed Musa (31),Mboke Samwel (26),Abdallah Kipaneli(25) na Mfaume Mussa (25).

Kamanda wa kanda hiyo Lazaro  Mambosasa amesema Julai 9, 2019 majira ya saa nane usiku huko maeneo ya Kibeberu na Magole  Ukonga watuhumiwa hao walivunja maduka matatu na kufanikiwa kuiba bidhaa mbalimbali, fedha pamoja na bajaji mbili zenye namba za usajili MC 312 CFB aina ya TVS na MC 540 CED aina ya TVS zote zikiwa na rangi ya bluu.  

Baada ya wizi huo taarifa zilipokelewa katika kituo cha Polisi Stakishari na upelelezi ulianza maramoja ambapo mnamo Julai 9, 2019 majira ya saa tano asubuhi watuhumiwa walikamatwa huko maeneo ya Hondogo Gogoni Kiluvya wilaya ya Ubungo.

Aidha watuhumiwa hawa wamekuwa wakifanya matukio ya uhalifu kwa kutumia gari aina ya Toyota Harrier  nyeusi yenye namba T.666 DJG ambayo inashikiliwa na Jeshi la Polisi ili kubaini mmiliki wake.

Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani hivi karibuni.

Updated: 11.07.2019 14:43
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.