Polisi wawili, afisa TRA wapandishwa kizimbani

Polisi wawili, afisa TRA wapandishwa kizimbani

10 June 2019 Monday 15:02
Polisi wawili, afisa TRA wapandishwa kizimbani

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
Ofisa Msaidizi wa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato nchini(TRA) Charity Ngalawa(28) na askari Polisi wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shtaka la  kuomba rushwa ya milioni 2.

Mbali na Ngawala washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai  ni askari Polisi  mwenye namba H 4810 PC Ramadhani Uweza( 28) na mwenzake H 4886 PC Simon Sugu( 26), wote kutoka Kituo cha Polisi Osterbay, wilaya ya Kinondoni.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na shtaka moja la  kuomba rushwa ya milioni 2 kutoka kwa mfanyabiashara wa Kariakoo, Ramadhani Ntunzwe.

Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili kutoka Takukuru, Sofia Gula amedai leo, Juni 10, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi,  kuwa washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 29, 2016 katika eneo la Kimara Mwisho, Wilaya ya Kinondoni.

Gula alidia  siku hiyo ya tukio, washtakiwa kwa pamoja wakiwa Watumishi wa Umma, walishawishi rushwa ya milioni 2 kutoka kwa mfanyabiashara Ramadhani Ntunzwe.

Gula alidia  washtakiwa hao walishawishi rushwa hiyo ili waweze kuachia  mizigo ya mfanyabiashara huyo  walioukamata kwa madai kuwa alifanya  udanganyifu wa bidhaa alizonazo na hivyo kuathiri ukadiriaji wa kodi, kazi ambayo ni ya mwajiriwa wake.

Washtakiwa baada ya kusomewa shtaka linalowakabili walikana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidia kuwa  upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo, wakili wa anayewatetea washtakiwa hao, Ambros Mkwera aliiomba mahakama iwape wateja wake dhamana kutoka na kesi inayowakabili kudhaminika.

Hakimu Shaidi, alitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa hao, ambayo ni kila mshtakiwa anatakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye barua inayotambuliwa kisheria pamoja na kitambulisho atakaye saini bondi ya milioni 5.

Washtakiwa wote wamefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huru kwa dhamana.

Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 10,2019, itakapotajwa na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.