Polisi yawahoji Steve Nyerere, Irene Uwoya  waachiwa kwa dhamana

Polisi yawahoji Steve Nyerere, Irene Uwoya  waachiwa kwa dhamana

19 July 2019 Friday 15:30
Polisi yawahoji Steve Nyerere, Irene Uwoya  waachiwa kwa dhamana

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewahoji na kuwaachia kwa dhamana wasanii wa filamu, Steve Nyerere na Irene Uwoya kutokana na kitendo cha kuwarushia fedha waandishi wa habari katika mkutano wao mapema wiki hii.

Kaimu kamanda wa kanda hiyo, Camilius Wambura amesema Julai 17, 2019 waliwahoji wasanii hao na kuwaachia kwa dhamana na kwamba uchunguzi unaendelea

''Tuliwaita baada ya kuonekana mmoja wao kwenye clip, yule Irene alionekana anatupa fedha  kwa wanahabari, na tuliwahoji na wapo nje kwa kudhaminiwa, uchunguzi mwingine unaendelea'' amesema Kamanda Wambura.

Julai 15,2019  Irene Uwoya, alionekana katika baadhi ya video zilizosambaa mitandaoni, akirusha fedha kwa wanahabari, kitendo kilichotafsiriwa ni udhalilishaji hata hivyo Irene alikiri kukosea na kuomba radhi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.