Raia wa Qatar azunguka Dunia kwa pikipiki

Raia wa Qatar azunguka Dunia kwa pikipiki

11 September 2019 Wednesday 16:42
Raia wa Qatar azunguka Dunia kwa pikipiki

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MWENDESHA pikipiki raia wa Qatar, Khalid Al Jabir amewasili nchini ikiwa ni sehemu ya kituo chake cha pili cha safari yake ya kuzunguka nchi sita barani Afrika.

Khalid anakuwa raia wa kwanza kutoka nchi za Kiarabu kusafiri kwa pikipiki kutoka jijini London(Uingereza) hadi Beijing nchini China

Pia ameweka rekodi ya kusafiri kutoka Alaska, Marekani hadi nchini Argentina safari iliyochukua urefu wa kilomita 40,000 kwa miezi mitano

Safari yake ya Afrika imeanzia nchini Kenya na itamalizika nchini Afrika Kusini.

Safari zake zinalenga kuhamasisha vijana kutembea sehemu mbalimbali na kuangalia maajabu ya Dunia pamoja na kutangaza utalii wa nchi husika

Safari yake ya Afrika itapita katika nchi ya Malawi, Zambia, Botswana na Namibia . Nchini Kenya amekaa kwa siku kumi na Tanzania pia atakaa kwa siku kumi. Akiwa mkoani Morogoro atagawa vifaa mbalimbali ikiwemo kompyuta mpakato(Laptop) katika moja ya shule mkoani humo.

‘‘Safari yangu ya kuanzia Kenya hadi Afrika Kusini ni safari yenye changamoto kwa kuwa ninakutana na kuona mambo mengi ikiwemo milima, mabonde, wanyama na mambo mengi ambayo kwa namna moja ama nyingine inaniongezea ujasiri na kuyajua vizuri mazingira ya Dunia,’’ amesema Khalid

Updated: 11.09.2019 16:51
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.