Rais Magufuli amhakikishia usalama Tshisekedi

Rais Magufuli amhakikishia usalama Tshisekedi

14 June 2019 Friday 08:44
Rais Magufuli amhakikishia usalama Tshisekedi

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
RAIS John  Magufuli amemuhakikishia rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo(DRC) Felix Tshisekedi kuwa Tanzania  haitayaondoa majeshi yake ya walinda amani kutoka DRC  hadi hapo  amani ya kudumu itakapopatika  nchini humo.

Walinda amani wa Tanzania wako DRC chini ya kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa cha kuimarisha amani kinachojulikana kama , 'Monusco.'
Rais Magufuli ametoa hakikisho hilo  Ikulu  Jijini Dar es Salaam Juni 13, 2019  katika hafla ya pamoja na  Tshisekedi ambaye yupo nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.

" Walinda amani wa Tanzania wataendelea kubakia huko hadi amani kamili itakaporejea nchini. Rais wa nchi mbili ni majirani, marafiki, makaka na madada,"alisema.

Dk Magufuli amesema  licha ya Tanzania kuwapoteza wanajeshi wake 30 wa kulinda amani nchini DRC, haitawaondoa wanajeshi wake huko.

Mwaka 2017 pekee walinda amani 12 wa Tanzania waliokuwa katika kikosi cha Umoja wa Mtaifa Monusco waliuwawa  baada ya kambi yao kuvamiwa mashariki mwa DRC, kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Tayari Tshisekedi  ameshafanya maridhiano na makundi kadhaa hasimu, na kuwafungua wafungwa wa kisiasa waliokuwa mahabusu. Hii ni hatua muhimu katika kurejesha amani nchini DRC

"Tanzania inaunga mkono juhudi za amani kwasababu hazitasaidia tu katika kuleta hakikisho la amani na uthabiti ; amani pia itachochea maendeleo ya kiuchumi baina ya nchi za maziwa makuu na bara zima la Afrika kwa ujumla ," alisema.

Kwa upande wake rais Tshisekedi amesema ziara yake nchini  imelenga  kuzungumza na rais Magufuli juu ya namna ya kufikia amani ya kudumu nchini DRC. Pia aliwashukuru walinda amani wa Tanzania wanaohudumu nchi yake chini ya mpango wa kikosi cha Umoja wa mataifa Monusco.

" Nimeongea na rais Magufuli kuhusu bandari ya Dar es Salaam port na Reli ya -Standard Gauge Railway (SGR) -ambayo imepangwa kufika Rwanda. Nilielezea kuhusu uwezekano wa kupanua zaidi mradi hadi DRC," alisema.
Amesisitiza kuwa ushirikiano wa kiuchumi wa mataifa ya Afrika utakaoleta maendeleo ya kudumu utafikiwa kupitia uwekezaji na utekelezwaji wa miradi ya miundombinu ,ikiwemo leri, barabara na nishati.

Rais Tshisekedi amefichua kuwa hivi karibuni DRC ilituma maombi ya uanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), hatua ambayo inaiondolea nchi hiyo vikwazo vya kibiashara

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.