Rais Magufuli apandisha cheo maafisa 9 magereza

Rais Magufuli apandisha cheo maafisa 9 magereza

02 June 2018 Saturday 13:30
Rais Magufuli apandisha cheo maafisa 9 magereza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wanne wa Jeshi la Magereza kutoka Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP) hadi kuwa Kamishna wa Magereza (Commissioner of Prisons – CP).

Maofisa hao ni Hamis Ngarama, Tusekile Mwaisabila, Augustine Sangalali Mboje na Gideon Marco Nkana.

Pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Magereza wengine 5 kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (Senior Assistant Commissioner of Prisons – SACP) hadi kuwa Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP).

Ambao ni Julius Mayenga Sang’udi, Afwilile Mwakijungu, John William Masunga, Phaustine Marint Kasike na Joram Yoram Katungi.

Uteuzi huo umefanyika mapema leo hii Juni 2, 2018.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.