Rais Magufuli ateua Mkurugenzi mpya wa Takukuru

Rais Magufuli ateua Mkurugenzi mpya wa Takukuru

06 September 2018 Thursday 12:50
Rais Magufuli ateua Mkurugenzi mpya wa Takukuru

RAIS John Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi, Diwani Athuman kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Taarifa ya uteuzi huo  imetolewa leo tarehe 6 Septemba, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.

Kamishna Diwani anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi, Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Balozi.

“Uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani unaanza leo tarehe 6 Septemba 2018,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Kamishna Diwani alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.