Rais Magufuli: Nitamkaba Lukuvi alipe pesa zangu

Rais Magufuli: Nitamkaba Lukuvi alipe pesa zangu

05 September 2018 Wednesday 16:09
Rais Magufuli: Nitamkaba Lukuvi alipe pesa zangu

RAIS John Magufuli amesema, atamkaba Waziri wa Ardhi, William Lukuvi ili amlipe Sh. 1 milioni fedha alizowapa wazee wawili ambao mmoja wao alidhulumiwa eneo lake.

Bibi Nyasasi Masige (mwenye kiwanja) akiwa na jirani yake wamemlalamikia Rais Magufuli kuwa, kuna tajiri aliyedhulimu kiwanja cha mmoja wao baada ya kumuuzia kiwanja cha pili kwa ajili ya kupata fedha za matibabu, na kwamba aliporudi kutoka kupata matibabu alikuta tajiri huyo amejimilikisha kiwanja cha pili.

Wazee hao walidai kuwa, mgogoro wao ulimfikia Waziri Lukuvi ambapo aliagiza bibi huyo kupatiwa kiwanja chake jambo ambalo halijafanyika hadi leo.

Kufuatia malalamiko hayo, Rais Magufuli alimtafuta Waziri Lukuvi kwa njia ya simu, na kumuagiza kumsimamisha kazi kamishna wa ardhi wa kanda hiyo kuanzia leo.

Baada ya hapo Rais Magufuli aliwakabidhi wazee hao kila mmoja Sh. 500,000 kutokana na usumbufu walioupata na kwamba, fedha hizo zitalipwa na Waziri Lukuvi. Rais Magufuli yupo mkoani Mara kwa ziara ya kikazi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.