Rais Tshisekedi kutua nchini leo

Rais Tshisekedi kutua nchini leo

13 June 2019 Thursday 07:03
Rais Tshisekedi kutua nchini leo

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC), Felix Tshisekedi Juni 13, 2019 anatarajia kufanya ziara ya kikazi kwa siku mbili nchini Tanzania.

Atapokelewa leo  na  mwenyeji wake  rais  Dkt. John Magufuli.

Akitoa taarifa ya ugeni huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda amesema rais F Tshisekedi atawasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere  majira ya mchana na baada ya kuwasili ataelekea Ikulu Dar es salaam ambapo atafanya mazungumzo na rais Dkt. John Magufuli kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kuimarisha uchumi na maendeleo.

Makonda amesema ugeni wa viongozi mbalimbali nchini ni matokeo ya uongozi imara na thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli katika usimamizi wa Amani, usalama, maendeleo na uwepo wa diplomasia imara.

Updated: 13.06.2019 07:09
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.