Rais wa Afrika Kusini atua nchini

Rais wa Afrika Kusini atua nchini

15 August 2019 Thursday 10:03
Rais wa Afrika Kusini atua nchini

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na mkewe Dk Tshepo Motsepe wamewasili nchini usiku wa kuamkia leo.

Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili kabla ya kuhudhuria mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini kwa Afrika (SADC)

Ziara yake itajikita zaidi katika kutembelea eneo la wapigania uhuru Mazimbu, Mkoani Morogoro, ili kujenga kumbukizi ya udungu kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

Aidha nchi 16 za SADC zimethibitisha kushiri mkutano huo wa 39 utakaofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 17 na 18, 2019.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi amesema maandalizi yamekalika na nchi ipo tayari kwa ugeni huo.

Mkutano huo ulitanguliwa na matukio mbalimbali ikiwemo maonesho ya wiki ya viwanda kutoka nchi wanachama wa SADC, Vikao vya Maafisa Waandamizi kutoka SADC, Vikao vya Mawaziri kutoka SADC na Mikutano mbalimbali ya sekta za SADC, ambapo maeneo haya yote Tanzania inachukua uenyekiti wa Nchi Wanachama.

Viongozi wakuu wengine wataanza kufika nchini kuanzia Agosti 15 na kuendelea. Agosti 17 na 18 Wakuu wa Nchi Wanachama watasaini mikataba mbalimbali na kuhitimisha ajenda zao.

PICHANI JUU: Rais Cyril Ramaphosa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Profesa Palamagamba Kabudi mara baada ya kutua nchini

PICHANI CHINI: Rais Cyril Ramaphosa na mkewe Dk  Tshepo Motsepe wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. 

Updated: 15.08.2019 10:17
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.