Reli ya kati kufungwa saa 72 kila wiki

Reli ya kati kufungwa saa 72 kila wiki

08 July 2019 Monday 08:38
Reli ya kati kufungwa saa 72 kila wiki

Na mwandishji wetu, Dar es Salaam
SHIRIKA la Reli Tanzania -TRC limetangaza kufunga njia ya Treni ya Kati kutoka Dar es Salaam hadi Isaka Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga kwa saa 72 kila wiki ambayo ni sawa na siku tatu kwa wiki ili kufanikisha ukarabati wa reli hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika, Ndugu Masanja Kungu Kadogosa, alisema kuwa ukarabati huo wa takribani kilometa 970 unaotarajia kuanza Julai 13, 2019 utachukua miezi mitatu zoezi ambalo kukamilika kwake kutaingiza faida mara dufu ya usafiri huo na kwa Taifa.

“Waandishi wa Habari na Watanzania kwa ujumla, TRC sasa tunakuja kuimarisha miundombinu ya Reli, tunafanya hivi kwa kuwa tunafahamu mnahitaji huduma hizi, tunaomba mtuvumilie kwa siku ambazo tutafunga njia hizi” alisema Ndugu Masanja Kungu Kadogosa.

Aidha alisema kuwa ukarabati huo ni pamoja na kubadilisha Mataluma na Reli kutoka ‘Pound 60 hadi Pound 80’ na kuunga maungio ya reli kwa umeme  ‘Flash Butt Welding’ ili kupunguza wizi wa vifungashio uliokuwa ukitokea siku za nyuma kwa kufungua bolt za viunganishio vya reli ‘fish plate’ katika maungio ya reli.

Alizitaja faida za ukarabati huo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa Speed ya Treni kutoka kilometa 35 kwa saa mpaka kilometa 75 kwa saa pamoja na kuongeza uwezo wa ubebaji mizigo kwa Exeli moja kutoka Tani 13 hadi 18.

‘’Baada ya kukamilika ukarabati huu Treni zetu zitaweza kubeba mizigo mingi zaidi kwa wakati mmoja, kwa haraka na usalama zaidi na pia itapunguza ajali za mara kwa mara, 

Lakini pia itaboresha mawasiliano na ishara za kuongezea Treni kwa kuweka mfumo wa kisasa ujulikanao kama ‘Train Warranty System’ ili kuondoa usumbufu wa mawasiliano kutoka kituo kimoja hadi kingine 

Hata hivyo  Masanja Kungu Kadogosa alisema kuwa ukarabati mwingine wa njia ya Reli kutoka Tanga kwenda Arusha ulianza mapema mwaka huu ambapo njia hiyo itaanza kutumika mwezi Desemba mwaka huu.

“Ndugu zangu wa mikoa ya Kaskazini mtaanza kunufaika na usafiri wa treni ya Abiria kuanzia Desemba mwaka huu, yaani Sikukuu za Krismas na Mwaka mpya mtaenda nyumbani na Treni ya Abiria ya TRC älisema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzani Ndugu Masanja Kungu Kadogosa.

Akizungumzia ujenzi wa Reli ya Standard Gauge inayoendelea kujengwa Nchini  Masanja Kungu Kadogosa alisema kwa awamu ya kwanza kutoka Dar Es Salaam kwenda Morogoro ujenzi huo umefikia asilimia 56.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.