Sababu ya JPM kwenda Afrika ya Kusini

Sababu ya JPM kwenda Afrika ya Kusini

24 May 2019 Friday 11:57
Sababu ya JPM kwenda Afrika ya Kusini
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
IMETAJWA kuwa sababu ya Rais John Magufuli kwenda nchini Afrika  Kusini ni kudumisha uhusiano wa kihistoria wa nchi hizo.

Mapema hii  leo Mei 24, 2019 rais Magufuli amesafiri kwenda nchini Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kuapishwa rais mteule wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa ambaye ataapishwa kesho, Mei 25, 2019
.
Pia Rais Magufuli atafanya ziara ya kitaifa nchini Namibia na atazindua mtaa  uliopewa jina la Mwalimu Nyerere ikiwa ni kutambua mchango alioutoa katika ukombozi wa taifa hilo.


Katika kuhudhuria sherehe za kuapishwa rais mteule Ramaphosa, rais Magufuli ameambatana  na rais mstaafu Jakaya Kikwete, Makamu mwenyekiti wa CCM bara, Philipo Mangula na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika  Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.

"Nchi ya Tanzania na Afrika ya Kusini zina uhusiano mkubwa na wa kihistoria na   kwamba Serikali na chama zina kila sababu ya kudumisha uhusiano na ushirikiano huo,'' amesema Kikwete

Viongozi hao wameondoka mapema leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kwa kutumia ndege la shirika la ndege Tanzania(ATCL)

Updated: 27.05.2019 14:48
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.