Sakata la Lissu: Mbowe asema tutareje tena Mahakamani

Sakata la Lissu: Mbowe asema tutareje tena Mahakamani

09 September 2019 Monday 14:53
Sakata la Lissu: Mbowe asema tutareje tena Mahakamani

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa chama cha Chadema, Freeman Mbowe amesema wanaenda kujipanga  na kurejea tena Mahakamani.

Mbowe ameyasema hayo leo Septemba 9,2019 mara baada ya uamuzi wa Mahakama kuu kukataa maombi ya Tundu Lissu ya kufungua maombi ya kibali cha kutengua uamuzi wa Spika wa Bunge Job Ndugai wa kumvua ubunge wa jimbo la Singida Mashariki.

Amesema kama chama  Mahakama ni chombo wanachokiamini  na wamesikia uamuzi wa jaji kuhusiana na kesi iliyokuwepo mahakamani hapo hivyo watarejea tena Mahakamani hapo.

"Ndugu yetu Lissu bado yupo nje ya nchi kwa matibabu tutafanya mawasiliano katika chama tutaendelea kutafuta haki hadi ipatikane" amesema Mbowe na kuongeza "Tunatambua haki haitapatikana kwa urahisi kwa sababu mbalimbali ila maamuzi yaliyotolewa kama chama tunayaheshimu."

Kiongozi huyo wa kambi ya Upinzani Bungeni amesema Mahakama ni chombo muhimu cha kutoa haki  na wataendelea kutumia kila mfumo kuhakikisha haki inatendeka.

"Katika Mahakama kuna ngazi mbalimbali zakupata haki hiyo  tutaendelea kutumia kila mfumo  wa kimahakama  kuhakakisha haki hiyo  inaendelea kupiganaiwa na kutafutwa,'' ameongeza.

Updated: 09.09.2019 15:05
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.