Sakata la wanafunzi Mbeya, Magufuli agongelea msumari

Sakata la wanafunzi Mbeya, Magufuli agongelea msumari

04 October 2019 Friday 15:32
Sakata la wanafunzi Mbeya, Magufuli agongelea msumari

Na mwandishi wetu, Songwe

RAIS John Magufuli ameagiza wanafunzi wote wa kidato cha tano na sita wa shule ya sekondari Kiwanja wilayani Chunya wafukuzwe shule na ili warejeshwe kila mzazi atoe fedha za ujenzi wa mabweni yaliyochomwa.

Pia ameagiza kuvunjwa kwa bodi ya shule hiyo

Ametoa maelekezo hayo leo Oktoba 4, 2019 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Wawa mkoani Songwe.

‘‘Nampongeza mkuu wa mkoa wa Mbeya(Chalamila) kwa uamuzi wake wa kuwacharaza viboko wanafunzi. Ninaagiza wanafunzi wote wa kidato cha tano na sita wafukuzwe shule, na ikitokea wanarejeshwa kila mzazi atoe fedha za ujenzi wa mabweni,’’ amesema Magufuli na kuongeza

‘‘Pia naangiza bodi ya shule hiyo ifutwe haraka iwezekanvyo kwa kuwa imezembea.’’

Maelekezo hayo ya Magufuli yanafuta sintofahamu iliyokuwa imetamalaki kwa watanzania ya hatua aliyokuwa amechukua mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ya kuwacharaza viboko wanafunzi 14 na kuamuru wanafunzi 392 wa kidato cha tano na sita Shule ya Sekondari Kiwanja wilayani Chunya kurudi nyumbani hadi Oktoba 18, 2019.

Alisema siku watakaporejea shuleni wanatakiwa kuwa na Tsh 200,000 kila mmoja kwa ajili ya ukarabati wa mabweni mawili ya shule hiyo yanayodaiwa kuchomwa moto na baadhi yao.

Alitoa uamuzi huo Oktoba 3, 2019 baada ya kufika katika shule hiyo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, siku moja baada ya kuwachapa viboko wanafunzi 14 wa shule hiyo kwa madai ya kuchoma moto mabweni ya shule hiyo.

Chalamila alisema wanafunzi ambao hatatekeleza amri yake ya kulipa fedha kupitia benki na kutofika shuleni Oktoba 18, 2019, atafuatwa nyumbani kwa pingu na hataruhusiwa kufanya mtihani wake wa mwisho.

Chalamila alisema wanafunzi 14 aliowachapa viboko ambao pia walikutwa na simu watatakiwa kulipa Tsh. 500,000 na watakaporejea shuleni waambatane na wazazi wao, kutaka fedha zote zipelekwe benki kabla ya Oktoba 18, 2019 na kupeleka risiti za malipo shuleni.

Updated: 04.10.2019 16:24
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.