Selasini wa Chadema amfagilia Naibu Waziri Ikupa kwa kuwa faraja

Selasini wa Chadema amfagilia Naibu Waziri Ikupa kwa kuwa faraja

06 June 2018 Wednesday 14:41
Selasini wa Chadema amfagilia Naibu Waziri Ikupa kwa kuwa faraja

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Rombo Joseph Selasini (Chadema) amempongeza Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Stella Ikupa kwa kuwa faraja kwa watu wenye ulemavu nchini Tanzania.

Selasini alitoa pongezi hizo bungeni leo jijini Dodoma alipopewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza ambapo alisema kuwa Naibu waziri Ikupa ambaye ni mlemavu, amekuwa faraja kwa wenzake na kumuombea aendelee kuwa hivyo hivyo.

Katika swali lake, Mbunge huyo alitaka kujua kama Naibu waziri huyo yupo tayari kwenda wilayani Rombo kutatua mgogoro kwenye chama cha walemavu.

Alisema kuwa mgogoro huo wa muda mrefu umesababisha wafadhili kujitoa na hivyo kusababisha shida kubwa kwa wananchama.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ikupa alimshukuru Mbunge huyo kwa kushugulikia matatizo ya walemavu kwenye jimbo lake.

Alisema kuwa mara baada ya kumalizika kwa kikao cha bunge la bajeti ataanza ziara kutembelea mikoa kadhaa, ikiwemo wilaya ya Rombo kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.

Akieleza kuhusu uteuzi wa baraza la walemavu, alisema kuwa ni kweli muda wa wajumbe umekwisha lakini serikali imekwisha anza mchakato wa kuwabadilisha.

Alisema kuwa waliandika barua kwa vyama vyote vya walemavu kwa lengo la kuwapatia majina ya watu wanaofaa kuingia kwenye baraza hilo.Aliongeza kuwa tayari Wizara imeyapokea majina na sasa ipo katika mchakato wa ndani.

Hata hivyo alibainisha kuwa serikali ina nia ya dhati kuhusu watu wenye ulemau na itaendelea kutoa ruzuku kupitia mfuko maalum ulioanzishwa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.