Serikali kufuta miliki, kuuza mali za wasiolipa kodi

Serikali kufuta miliki, kuuza mali za wasiolipa kodi

11 June 2019 Tuesday 10:57
Serikali kufuta miliki, kuuza mali za wasiolipa kodi


Na mwandishi wetu, Dodoma
SERIKALI imesema ifikapo Juni 20, 2019 itakuwa mwisho wa ulipaji madeni ya kodi ya ardhi na majengo na kwamba hatua za kisheria ikiwamo kufuta umiliki na uuzaji mali zitachukuliwa.

Msimamo huo umetolewa leo Juni 11, 2019 mjini Dodoma na waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Amesema hayo katika mkutano wake  na wamiliki binafsi, watendaji wa taasisi na mashirika  yenye madeni .


"Ifikapo Juni 20, 2019 kila mtu, taasisi, mashirika yote yanayodaiwa kodi ya ardhi na pango yawe yamekamilisha kulipa madeni wanayodaiwa. Ikipita hapo hatua za kisheria ikiwemo ufutaji miliki, uuzaji wa vitu, ardhi utafanyika,'' amesema Lukuvi

Amesema hadi sasa hakuna taasisi, wala mashirika yaliyoomba msamaha wa kufutiwa madeni na kwamba wafanye hivyo kwa mujibu wa taratibu.

Katika mkutano wake huo wa leo jumla ya mashirika na taasisi 207 yaliyaalikwa na kwamba serikali inatarajia kupata zaidi ya takribani bilioni 200 za kodi ya pango na ardhi nchini kote ambazo ni madeni.

Updated: 11.06.2019 17:45
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.