Serikali yaagiza pacha walioungana kuletwa Dar haraka, kutenganishwa

Serikali yaagiza pacha walioungana kuletwa Dar haraka, kutenganishwa

05 June 2018 Tuesday 12:53
Serikali yaagiza pacha walioungana kuletwa Dar haraka, kutenganishwa

Na Mwandishi Wetu

WIZARA ya afya imeagiza watoto mapacha waliozaliwa huku wakiwa wameungana huko mkoani Kagera kuletwa haraka kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kuwatenganisha.

Agizo hilo limetolewa bungeni leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Suzan Lyimo (Chadema).

Mbunge huyo alisema kuwa huko Kyaka kuna watoto wamezaliwa huku wakiwa wameungana na kama serikali ina taarifa.

“Je taarifa hii serikali inayo na hatua gani zimechukuliwa isije ikatokea kama kwa Consolata na Maria,” alisema.

Consolata na Maria ni pacha waliozaliwa huku wameungana huko mkoani Iringa, wameishi kwa kipindi cha miaka ishirini, na kufariki juzi wanatarajiwa kuzikwa kesho.

Akijibu swali hilo Waziri Ummy Mwalimu alisema kuwa ni kweli serikali ina taarifa za watoto hao na tayari imekwisha toa maagizo.

Alisema kuwa serikali imetoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Hospitali mkoani Kagera kufanya utaratibu wa kuwaleta watoto hao kwenye hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya hatua za kuwatenganisha.

Alisema kuwa jopo la watalaam watakaa na kuangalia namna ya kuwatengenisha watoto hao ndani au nje ya nchi.

Aidha aliwataka wazazi wanaojifungua watoto ambao si wa kawaida kuwasiliana na mamlaka husika kwa ajili ya msaada zaidi.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.