Serikali yaanza kulipa fidia ujenzi wa bandari kavu huko Mbeya, bunge laambiwa

Serikali yaanza kulipa fidia ujenzi wa bandari kavu huko Mbeya, bunge laambiwa

01 June 2018 Friday 10:11
Serikali yaanza kulipa fidia ujenzi wa bandari kavu huko Mbeya, bunge laambiwa

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema nia ya kujenga bandari kavu katika jiji la Mbeya bado ipo kwani suala hilo ni la kimkakati na sasa imeanza kuchukua hatua.

Hayo yamebainishwa bungeni na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye alipokuwa akijibu swali na Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza (CCM).

Mbunge huyo aliitaka serikali kueleza lini ujenzi wa Bandari kavu katika mkoa wa Mbeya utaanza.

Akijibu Naibu Waziri Nditiye, alisema kuwa ni kweli serikali imechukua eneo huko Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu.

Alisema kuwa kwa sasa wameanza kulipa fidia kwa ajili ya wananchi waliopisha eneo la mradi na kazi hiyo ikikamilika wataanza shughuli za ujenzi.

Aliongeza kuwa bandari hiyo ni ya kimkakati na itasaidia kusafirisha mizigo itakayokuwa ikielekea nchi jirani za Malawi, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya watu wa Kongo.

Wakati huo Nditite amsema kuwa serikali ina mpango wa kuboresha miundombinu ya Ziwa Nyasa ili kuwawezesha wananchi kunufaika nalo.

Alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Ludewa Deo Ngalawa (CCM) aliyetaka kujua kujenga ghati nyingi katika ziwa hilo ili kuwapunguzia kero ya vituo wasafiri.

Akijibu Naibu waziri Nditiye, alisema serikali imetenga fedha kwa ajili ya uimarishaji wa bandari za Matema, Kiwira, Lupingu na tayari zabuni za usanifu na mkandarasi ilitangazwa.

Aliongeza kuwa kazi ya mshauri mwelekezi itakamilika mwaka huu , ambapo ujenzi wa ghati katika vijiji vya Nkanda, Masele, Iyiga  utaanza.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.