banner68

Serikali yakiri matumizi mabaya ya misitu, kuwachukulia hatua kali wahusika

Serikali yakiri matumizi mabaya ya misitu, kuwachukulia hatua kali wahusika

12 June 2018 Tuesday 13:53
Serikali yakiri matumizi mabaya ya misitu, kuwachukulia hatua kali wahusika

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imekiri kuwa kuna matumizi mabaya ya misitu baadhi ya maeneo na kuagiza hatua kuchukuliwa dhidi ya wahusika, Naibu waziri wa Mali Asili na Utalii, Japhet Hasunga ameliambia Bunge.

Alikuwa akijbu swali la nyongeza la Mbunge wa Kaliua Madgalena Sakaya (CUF) aliyetaka kujua sababu za serikali kuhalalisha kuvuna mazao ya misitu maeneo hakuna miti.

Aidha alisema kuwa kuna maafisa misitu ambao kazi yao imekuwa ni kutembea na mihuri na kugonga magogo bila kuzingatia ilipotoka.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Hasunga, aliiri kuwa ni kweli kuna matumizi mabaya ya misitu katika vituo kadhaa.

Alisema kuwa na eneo la kuvuna misitu hakuna tatizo, lakini shida ni pale jinsi mazao ya misitu ule yanavyopatikana.

Akitolea mfano alisema kuwa endapo mvunaji wa mkaa atakuwa na vibali vyote hilo halina shida, kinyume chake achukuliwe hatua.

Aidha alisema kuwa wakala wa misitu nchini (TFS) imepewa kazi ya kulinda na kusimamia hifadhi za misitu kutoingiliwa bila kibala maalum.

Alisema kuwa wakala hiyo ina eneo hekta za miyi milioni 15.4 au asilimia 38 ya nchi.

Aliongeza kuwa Tamisemi na serikali za vjiji zimepewa hekari zao kwa ajili ya kuzitunza.

Alibainisha kuwa TFS imekuwa ikifanya kazi ya kusavei na kuimarisha mipaka ambapo hadi sasa tayari kilomita 13100 zimekwisha safishwa, maeneo mengine kuwekewa vigingi na kupanda miti kwenye mipaka.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.