banner68
banner58

Serikali yapitisha kanuni mpya mifuko ya hifadhi ya jamii

Serikali yapitisha kanuni mpya mifuko ya hifadhi ya jamii

06 September 2018 Thursday 18:19
Serikali yapitisha kanuni mpya mifuko ya hifadhi ya jamii

Baada ya kuunganisha mifuko minne ya hifadhi ya jamii Serikali imetoa kanuni mpya zinazozuia fao la kukosa ajira. 

Kwa mwanachama atakayeachishwa kazi, kanuni zinasema atalipwa fao la kutokuwa na ajira ambalo ni sawa na theluthi moja (asilimia 33.3) ya mshahara aliokuwa anapokea akiwa kazini. 

Kuhusu malipo hayo kanuni hizo zinasema, “yatadumu hadi miezi sita ndani ya mwaka mmoja mpaka mwanachama huyo atakapopata ajira nyingine. Endapo hatopata ajira mpya, mwanachama hatolipwa kwa zaidi ya miezi 18 kwa muda wote wa utekelezaji wa taaluma yake.” 

Baada ya Bunge kupitisha Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na kuiunganisha mifuko ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF na kuunda mmoja kwa ajili ya watumishi wa umma ambao umeanza kufanyakazi kuanzia Agosti Mosi, 2018 kanuni mpya zimepitishwa.

Kabla ya kuunganishwa kwa mifuko hiyo, kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu fao la kujitoa ambao hata hivyo, Serikali ilishikilia  msimamo wa kuliondoa.

Agosti 17, Waziri Jenista Mhagama mwenye dhamana ya kazi na ajira nchini amesaini kanuni za Sheria ya Hifadhi ya Jamii kuruhusu kuanza kutumika kwake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Suimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii, Irene Kisaka alithibitisha: “Ni zenyewe. Zimepitishwa na zitaanza kutumika.” 

Ikitokea mwanachama huyo hajapata ajira nyingine miezi 18 baada ya kupokea malipo ya kutokuwa na ajira basi atatakiwa kubadili michango yake kwenda mpango wowote wa kuchangia kwa hiyari aupendao. 

Kiwango kitakachohamishwa kwenda mpango huo kitakuwa jumla ya michango yote kutoa pensheni aliyolipwa kipindi cha kukosa ajira. Mwanachama huyo ataendelea kuchangia mpango aliouchagua kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazousimamia. 

Utaratibu wa fao la kukosa ajira linawahusu wale wanaofanyakazi za muda mfupi au za mkataba pia. Kwa mwanachama ambaye michango yake ni chini ya miezi 18 ambayo ni sawa na mwaka mmoja na nusu kanuni zinasema anastahili malipo ya pamoja kiasi cha asilimia 50 baada ya kuachishwa kazi. 

Endapo ataendelea kukosa ajira kwa miezi 18 baada ya kupokea asilimia 50 ya michango yake, atatakiwa kujiunga na mpango wowote wa kuchangia kwa hiyari atakaoupenda. 

“Kiasi kitachopelekwa kwenye mchango wa hiyari kitakuwa kilichobaki baada ya malipo ya awali, asilimia 50,” zinabainisha kanuni hizo. 

Kama ilivyokuwa awali, kanuni zinasema mwanachama atastahili pensheni endapo atakuwa amechangia kwa kipindi kisichopungua miezi 180 au miaka 15. 

Na yule atakayekuwa amechangia kwa kipindi hicho au zaidi lakini akaachishwa kazi kwa manufaa ya umma kabla ya kufikisha umri wa kustaafu, atalipwa kiinua mgongo lakini ataanza kupokea pensheni ya kila mwezi atakapofikisha umri unaokubalika.

Kanuni hizo zinatambua miaka 55 kuwa ndio umri wa kustaafu kwa hiyari na 60 kwa mujibu wa sheria. 

Na mwanachama atakayeachishwa kazi kabla ya kufikisha umri wa kustaafu lakini amechangia chini ya miaka 15 au miezi 180, atalipwa kiinua mgongo pekee. 

Uteuzi

Mwanachana ambaye amechangia kwa zaidi ya miezi 180 lakini hajafikisha umri wa kustaafu ila ameteuliwa kushika wadhifa wa kisiasa ambako kuna utaratibu maalumu kwa ajili yao, basi atalipwa kiinua mgongo wakati akisubiri kupokea pensheni atakapofikisha miaka 55. 

Licha ya watakaoteuliwa, ikitokea mwanachama ameapunguzwa kazi, ofisi aliyokuwa anahudumu imefutwa au imefanyiwa marekesho hiyo nafasi yake imeondolewa lakini amechangia kwa muda huo, naye atakuwa na haki ya kupata kiinua mgongo na kusubiri pensheni atakapofikisha umri unaokubalika. 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Nehemia Nyangwa 2018-09-12 22:31:41

Mim naomba kuuliza kama unasema anayetakiwa kujaza yaan mafao ya kujitoa ni mfanyakaz aliyefikisha umri wa kustafu.
sas je sis temporary na season ambao hatuna mkataba wa kudumu mnatusaidiaje maana siwez kuacha 120000 halafu nikangoja mpaka miaka 60 mbna vigum sana.