Serikali yatoa neno kwa Watanzania

Serikali yatoa neno kwa Watanzania

30 May 2019 Thursday 15:19
Serikali yatoa neno kwa Watanzania

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MKURUGENZI wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi leo Mei 30,2019  jijini Dar es Salaam ametoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya utekelezaji wa serikali wa hadi kufikia Mei, 2019 kama ifuatavyo:

KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI •  Kwa kuwa leo zimebai chini ya saa 48 kabla ya kufika Juni Mosi, 2019, nisisitize kwa Watanzania na wadau wote kuwa katazo la kuingiza, kusafirisha nje, kutengeneza hapa nchini, kutumia na kuingiza nchini mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku liko pale pale na usisubiri saa ifike, chukua hatua sasa;

• Baada ya bashrafu hii, kama nilivyosema leo nina mambo makuu matatu ya kuwaeleza kuhusu yanayoendelea na yanayotokea Serikalini katika utekelezaji wa ahadi, mipango na mikakati ya Serikali kama ifuatavyo:


1. ZIARA ZA RAIS NJE YA NCHI • Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano, kwa takribani wiki moja sasa amekuwa ziarani katika nchi kadhaa za Afrika akianzia Afrika Kusini, Namibia na sasa amekamilisha ziara nchini Zimbabwe;


• Ziara katika nchi hizi wanachama wa SADC ilikuwa muhimu kwa sababu pamoja na uhusiano wa kipekee na kihistoria wa Tanzania na nchi hizo, mfahamu kwamba baada ya miaka 16, kuanzia Julai mwaka huu, Tanzania itashika Uenyekiti wa SADC na itakuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa SADC Agosti, 2019


ZIARA YA RAIS NJE YA NCHI… • Pamoja na kuimarisha Ushirikiano na urafiki uliopo kati ya Tanzania, Afrika Kusini, Namibia na Zimbabwe, ziara hii pia imekuwa na mafanikio yafuatayo katika Diplomasia ya Uchumi:


• 1. Uwekezaji, masoko na biashara: Kupitia ziara hii, Tanzania imefikia makubaliano kadhaa yatakayoiwezesha nchi yetu kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji na mataifa yote matatu. Aidha, Tanzania imepata soko la mahindi tani 700,000 nchini Zimbabwe na maeneo mengine ya ushirikiano katika kilimo, utalii, usafiri wa anga, miundombinu pia yamefikiwa na/au yatajadiliwa zaidi kupitia Tume za Ushirikiano wa Pamoja (JPCs).


MANUFAA ZIARA YA RAIS… • 2. Fursa kwa lugha ya Kiswahili: Akiwa ziarani, Mhe. Rais ametumia fursa ya uhitaji uliopo hasa nchini Afrika Kusini na Namibia wa walimu wa lugha ya Kiswahili, kwa kufikia mazungumzo ya awali ili baadaye walimu wa Tanzania ambao ndio manju, galacha na nguli wa asili wa lugha adhimu ya Kiswahili wapate fursa ya ajira katika nchi hizo;


• Niseme tu kufuatia kazi kubwa aliyoifanya Rais, niwatoe wasiwasi, ukiacha ubauji wetu katika lugha hii aushi ya Kiswahili, tayari kama Taifa tumeanza kufanya Ithibati ya Wataalamu bingwa wa kufundisha Kiswahili. Hadi sasa, BAKITA imewathibitisha wataalamu 708 ambao ni walimu na wakalimani wa Kiswahili na wako kwenye Kanzidata ya Kitaifa ya Watalaamu wa Kiswahili. Kujisajili ingia www.lugha.bakita.go.tz au www.bakita.go.tz •


2. MAGEUZI SEKTA YA MADINI YAANZA KUWA BARAKA  • Ndugu waandishi wa habari; • Eneo la pili la muhimu leo wananchi kujua kwa kina kinachoendelea ni mageuzi ambayo wengi wamekuwa wakiyasikia kuwa yanatokea katika sekta muhimu ya madini. Swali kuu ni Je, vita hii tunashinda au tunaanguka?;


• TUNASHINDA: Katika sekta ya Madini Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mageuzi mbalimbali ikiwemo kutunga Sheria Mpya za Madini, kurekebisha za zamani ikiwemo marekebisho makubwa ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2017 ambapo iliundwa taasisi mpya ya Tume ya Madini.


SEKTA TA MADINI…TUNASHINDA • 1.Sifa kwa Taifa: Mabadiliko haya yameanza kuleta faida kwa Nchi ambapo kwa sasa Tanzania inasifika duniani kama nchi ambayo inageuza “laana” ya madini kuwa “Baraka” ya Madini na nchi nyingi za Afrika zimeanza kuiga mageuzi tunayoyafanya ikiwemo kupitia upya mikataba na wawekezaji na pia watafiti mbalimbali wanairejea Tanzania katika hili;


• 2. Masoko ya Madini Yaanza: Baada ya takribani miaka 10 ya tamko katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 la kuanzisha masoko ya madini kukwama, hatimaye Januari mwaka huu, Rais Magufuli alitoa agizo na sasa limetekelezwa. Masoko haya ni vituo vya kuthibiti ubora, thamani na takwimu za madini. Mpaka Mei 29, 2019 masoko 24 yalishafunguliwa na kuanza kazi.

MASOKO NI CHACHU YA MAPATO • Mfano wa Mkoa wa Geita: Soko hili la kwanza nchini lilianza rasmi Machi 17, 2019: • Takwimu za jumla ya uzalishaji wa miezi miwili kabla ya kuanza Soko la Geita, zinaonesha kuwa uzalishaji wa dhahabu uliorekodiwa ulikuwa ni jumla ya kilogramu 259.12;


• Takwimu za jumla ya uzalishaji wa dhahbu kwa miezi miwili baada ya kuanza Soko la Madini Geita, zinaonesha uzalishaji umeongezeka kwa kiasi kikubwa na kufikia kilogramu 312.65 za dhahabu huku mwezi April, 2019 pekee ukiweka rekodi ya Geita kwa kuzalisha kilogramu 200 ambazo hazijapata kufikiwa mkoani humo kwa wachimbaji wadogo na wa kati.


MAPATO ZAIDI YAMIMINIKA…. • 3. Mapato Sekta ya Madini Yanamiminika: Tunaweza kujinasibu kwa yote katika mageuzi ya sekta ya madini; sheria mpya, masoko na udhibiti wa utoroshaji, lakini nafahamu watanzania wengi wanataka kuona ni kwa kiwango gani tumeanza kufaidika na madini kutoka “laana” hadi “baraka”?


• Takwimu za mpaka Mei, 2019 zinazidi kuthibitisha kuwa Watanzania wanapaswa kuendelea kumuombea na kumuunga mkono Rais Magufuli kwani mawazo, nia yake na miongozo yake katika sekta hii ni ushahidi mwingine kuwa FALSAFA za Rais Magufuli zisizo na mawaa zinailetea mafanikio makubwa. Makusanyo ya miezi 11 mwaka huu yameshazidi ya mwaka jana kama ifuatavyo:

Uzalishaji na Mapato ya Tanzanite Vyaongezeka:
• Tangu Serikali ilipoamua kujenga ukuta kuzunguka eneo la wachimbaji na kisha kuweka mifumo ya masoko na ukaguzi humo humo ndani, uzalishaji na mapato ya Serikali kutoka kwa wachimbaji wadogo vimeongezeka kwa kiwango cha kuridhisha kama ifuatavyo

SOKO LA DHAHABU CHUNYA • Mtakumbuka kuwa hivi karibuni Mhe. Rais alipokuwa ziarani Mbeya na alipofika Chunya aliagiza haraka soko la madini lianze, kwanza niwajulishe kuwa soko hilo limeanza rasmi tangu Mei 2, 2019 na tayari limeanza kuonesha mafanikio kama ifuatavyo:


• Mwezi Machi kabla ya soko uzalishaji ulikuwa takribani kilogramu 29.02 na Serikali ilikuwa ikipata mapato ya TZS milioni 173.53. Siku 28 tangu soko lianze uzalishaji umepanda kilogramu 100.22 na mapato yameongezeka hadi kufikia TZS milioni 588.91 .


MIFUMO YA KIDIGITALI YA MAPATO YALETA MAFANIKIO MAKUBWA • Ndugu Waandishi wa Habari; • Mnafahamu kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imewekeza sana msisitizo katika kukusanya mapato lakini na si tu kukusanya mapato bali pia kutumia mifumo ya kisasa itakayoongeza Ufanisi;


• Tayari Serikali ilishazindua mifumo kama ule wa kufuatilia miamala ya simu (TTMS), Mfumo Mkuu wa Mapato ya Serikali (GePG) na mingine mingi.


MFUMO WA TTMS • “Telecommunications Traffic Monitoring System” (TTMS) ni Mfumo wenye uwezo wa kubaini takwimu mbalimbali zinazopita katika mitandao ya mawasiliano. Mfumo huu baada ya mwekezaji kuusimamia kwa miaka mitano Januari, 2019 Rais aliupokea rasmi na sasa uko chini ya Serikali;


• Mfumo huu unasaidia Serikali kujua mapato ya kampuni za simu na mapato yanayotokana na mifumo ya kutuma na kupokea fedha.


MAFANIKIO YA TTMS • Kabla ya Mfumo wa TTMS Serikali ilikuwa haipati kitu kabisa katika miito ya simu za nje wala kuwa na uwezowa kuhakiki mapato ya simu za ndani katika kuapata mapato stahiki katika miamala ya fedha kwa njiia ya simu za mkononi;


• Tangu mfumo wa TTMS ulipofungwa kwa eneo la mapato ya simu za nje tu, Serikali imekwishakusanyaTZS. Bilioni 97.16 ikiwa ni malipo ya kodi zitokanazona mapato ya kampuni za simu kwa simu za kimataifa zinazoingiana kuishia hapa nchini.


• Aidha, kwa idadi ya miamala ya fedha kwa njia ya simu kati ya Julai, 2018 na Machi, 2019, uhakiki wa TTMS umeonesha kuongezeka kwa miaka kutoka miamala bilioni 1.94 hadi miamala bilioni 2.26 na hii inamaanisha Serikali inapata kodi zaidi, jambo ambalo kabla ya mfumo ilikuwa ngumu kujua.


MFUMO WA MAKUSANYO YA MAPATO YA SERIKALI GePG • GePG ni kifupi cha “Government e-Payment Gateway System”. Huu ni Mfumo wa kielektroniki unaowezesha ukusanyaji wa fedha za umma kielektroniki Serikalini.;


• Mfumo huu umebuniwa na kutengenezwa na wataalamu wa ndani wa Serikali. Mfumo wa GePG unasimamiwa na Wizara ya Fedha na Mipangokiufundi na kiundeshaji.


• Miundombinu ya mfumo huu imesimikwa kwenye kituo cha kuhifadhi DATA cha Serikali (Government Data Center) na inasimamiwa na wataalamu wa Kitanzania.


TAASISI ZILIZOUNGANISHWA GePG
Taasisi mbalimbali za umma zimeendelea kuunganishwa na Mfumo wa GePG ili kukidhi matakwa ya Sheria ya Fedha za Umma lakini pia kuongeza ufanisi.
Mpaka tarehe 29 Mei, 2019, idadi ya taasisi zilizounganishwa na kutumia Mfumo kukusanya Fedha za Umma ni 430. Taasisi zilizounganishwa ni pamoja na Halmashauri zote nchini ambazo ni 185.

Updated: 31.05.2019 09:05
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Yusufu Rajabu Kanyama 2019-06-01 20:05:50

Kazi nzuri ya Serikali ya awamu ya tano inaonekana wazi. Sasa mkazo uwekwe kwenye kilimo. Tuachane na kilimo cha kukidhi njaa tujikite kwenye kilimo biashara.