Serikali yatoa ruksa kwa watumishi kuomba uhamisho

"Uhamisho huo haujalishi una muda gani kazini, pia waliotuma barua zao kabla au baada ya kusitishwa uhamisho huo watume tena barua zao na zitajibiwa"

Serikali yatoa ruksa kwa watumishi kuomba uhamisho

"Uhamisho huo haujalishi una muda gani kazini, pia waliotuma barua zao kabla au baada ya kusitishwa uhamisho huo watume tena barua zao na zitajibiwa"

03 June 2019 Monday 04:56
Serikali yatoa ruksa kwa watumishi kuomba uhamisho

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

SERIKALI imetangaza rasmi ruksa kwa watumishi wa serikali, kuomba  ruhusa ya uhamisho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa  inawataka watumishi wa serikali za mitaa kuwa uhamisho uliositishwa sasa umefunguliwa rasmi Juni 1, 2018.

Inaeleza kuwa uhamisho huo haujalishi una muda gani kazini, pia waliotuma barua zao kabla au baada ya kusitishwa uhamisho huo watume tena barua zao na zitajibiwa.

Barua hizo zimetakiwa  kutumwa moja kwa moja kupitia barua pepe(email) kwa katibu mkuu Tamisemi pasipo kupitia sehemu yoyote ili kusiwepo na  urasimu wowote.
'' Pia imemtaka muombaji  kuweka namba yake ya simu ya mkononi na barua pepe(email) kama anayo." 

Takribani miaka mitatu iliyopita serikali ilitangaza kusimamisha kwa muda zoezi la uhamisho kwa watumishi wa umma.
Uamuzi huo ulizua sintofahamu kwa watumishi wakidai  kukaa mbali na familia ni jaribu lingine katika maisha kwa gharama za maisha kuwa juu kutokana na matumizi kuongezeka.

Kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa kuleta migogoro katika ndoa hasa ya kimahusiano na kimapenzi 

Pamoja na  familia kukosa huduma za wazazi wote wawili.

Updated: 03.06.2019 09:06
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
misha 2019-06-06 07:50:05

hii habari ni ya mwaka huu 2019 au 2018?

Avatar
misha 2019-06-06 07:50:20

hii habari ni ya mwaka huu 2019 au 2018?

Avatar
Mwamba 2019-06-19 07:41:25

Hii Habr N Ya Mwaka Huu Wa 19 Au Mwaka Jana ?

Avatar
kamala 2019-07-09 08:07:52

mwaka 2018