SERIKALI:Wakuu mikoa, wilaya msiwazuie wakulima kuuza mazao yao

SERIKALI:Wakuu mikoa, wilaya msiwazuie wakulima kuuza mazao yao

05 August 2019 Monday 11:45
SERIKALI:Wakuu mikoa, wilaya msiwazuie wakulima kuuza mazao yao

Na mwandishi wetu, Mwanza

SERIKALI imepiga marufuku kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuwazuia wakulima kuuza chakula chao kwa kuhofia uwepo wa njaa. Vilevile imesema inajiandaa kuifanyia mabadiliko sera ya kilimo ya mwaka 2013 ili kuondoa changamoto na vikwazo kwa wakulima

Msimamo huo umetangzwa  jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe  wakati akifungua sherehe za wakulima  na maonyesho ya kilimo (Nanenane) katika viwanja vya Nyamhongolo mkoani Mwanza.

Alisema kila mkulima, anajua namna anavyotunza  na kuilisha familia yake hivyo  kama kuna kiongozi anahofia uwepo wa njaa ni vema  akanunua mazao hayo  kwa bei anayotaka mkulima na kuyatunza ili yaweze kusubiria dhana aliyoiweka kichwani kwamba kutakuwapo na uhaba wa chakula.

“Hatuwezi kujenga viwanda wakati wakulima ni masikini wa kutupwa,  lazima tuwawezeshe kwa kutengeneza mazingira ya watu kunufaika na kilimo chao sambamba na kuwa na soko la uhakika, ndio maana leo hii kama wizara tumeanza kupitia sera ya kilimo na kuondoa changamoto  na  vikwazo vilivyokwekwa .

“Sera iliyopo imepitwa na wakati  kabisa,  inawaumiza wakulima na kuwafanya kubaki  kila mwaka kuilisha nchi na matajiri huku wao wakibaki na umasikini wao  huku kukiwapo na utitiri wa taasisi nyingi ambazo ukichunguza zimeanzishwa kwa lengo la kuwakandamiza, hii haiwezekani kama wizara tumeanza kuangalia ni taasisi gani zinatakiwa  kufutwa na kubaki  chache.

“Fedha ambazo zilikuwa zikielekezwa kwenye utitiri wa taasisi hizo, zitaelekezwa katika mfuko maalum  ambo  wizara tunatarajia kuanzisha  na kazi ya mfuko huo ni kufidia mkulima pale inapotokea mtikisiko wa bei katika soko la dunia, kama serikali hatuna uwezo wa kuthibiti bei ya soko la dunia, mfuko huo ndio utakaokuwa na kazi ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuwafikia wakulima,”alisema.

Alisema Serikali ilikuwa ikipokea fedha nyingi kutoka mataifa ya nje ili kuendeleza kilimo, lakini zilikuwa zikishia katika semina mafunzo kwa  watendaji, huku  asilimia 50 ya fedha zilizokuwa zikipokelewa ndizo  zinafika kwa wakulima.

Alisema  alitoa mfano, mtikisiko uliotokea katika pamba na korosho  mwaka huu, kama Serikali  isingechukua hatua ya kuzungumza na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutoa fedha za kununulia pamba,  basi  wangeuza kilo moja  kati ya Sh 500- 700 kulingana na bei ya soko la dunia.

Alisema tayari vikao kati ya Serikali na BoT vya kutoa fedha za pamba vimekamilika juzi na kuanzia leo Jumatatu fedha zitaanza kutolewa katika benki zingine kwa ajili ya kulipa wakulima wa pamba ambapo tayari bei elekezi ni Sh 1,200 kwa kilo moja.

“Ichukulieni hali  hali ya usafirishaji wa pamba kutoka mikononi mwa wakulima kama dharura maana mvua ikianza kunyesha zao hilo likiwa bado lipo majumbamni ni hasara, niwaambie baada ya kupitisha sera mpya na kuunda mfuko wa fidia kwa wakulima, hakika suala kama lililojitokeza katika korosho na pamba litakuwa historia na halitajitokeza maana Serikali tumejipanga kuchukua hatua.

“Mbali ya mfuko wa fidia, kama wizara tumebaini kuwapo na kasoro kadhaa katika bodi ya pamba hivyo kama Serikali  tunaiagiza bodi ya pamba kuanza mchakato wa kuainisha mahitaji yote ya wakulima kisha tutakuja na mfuko fulani  wa uagizaji pembajeo kwa pamoja, lengo ni kupunguza hasara kwa mkulima,”alisema.

Wakati huo huo, Bashe aliwaagiza wakuu wa wilaya, mikoa na watendaji wengine wanaohusika na sekta ya kilimo kuhakikisha mwaka huu wakulima hawapandi pamba kwa kumwaga mbegu, isipokuwa  kwa kutumia kamba lengo ni kulima kisasa na kupata mavuno mengi.

Updated: 05.08.2019 15:13
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.