banner68
banner58

Shaffih Dauda, MC Luvanda washikiliwa na polisi

Shaffih Dauda, MC Luvanda washikiliwa na polisi

19 September 2018 Wednesday 07:05
Shaffih Dauda, MC Luvanda washikiliwa na polisi

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wanadaiwa kuwashikilia mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Clouds, Shaffih Dauda na MC Luvanda kwa kile kinachodaiwa kumiliki mitandao ya Youtube bila kusajili maudhui.

Mwingine aliyekamatwa katika sakata hilo ni pamoja na msimamizi wa mtandao wa Youtube wa Shaffih, anayejukana kwa jina Ben Ali, maarufu kwa jina la Ben On Air.

Taarifa iliyopatikana usiku huu wa Septemba 18, kutoka kwa watu wa karibu wa Shaffih zinadai mtangazaji huyo na wenzake hao walikamatwa tangu Ijumaa iliyopita na kufikishwa kituo cha polisi cha Mabatini kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi  wanakoshikiliwa hadi sasa.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.