Shafii Dauda, mwezake kusomewa mashtaka ya awali

Shafii Dauda, mwezake kusomewa mashtaka ya awali

12 June 2019 Wednesday 16:34
Shafii Dauda, mwezake kusomewa mashtaka ya awali

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Julai 10, 2019 kumsomea maelezo ya awali( PH) mmiliki wa Mtandao wa Shafii Dauda, Shafii Dauda Kajuna na mwenzake, Benedict Kadege.

Shafii na mwenzake, wakabiliwa na shtaka moja ya kutumia maudhui ya Mtandao bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini ( TCRA).

Uamuzi huyo umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina, baada ya upande ukiongozwa na Wakili Jenifer Massue kuieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri hilo kukamilika.   

Baada ya maelezo hayo, hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 10, 2019, itakapokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa hoja za awali.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Shafii na Kadege wanadaiwa  kati ya Juni 14 hadi Septemba, 2018, ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la Shafii Dauda, walitoa maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali kutoka mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Updated: 12.06.2019 16:54
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.