Shamim, mumewe waendelea kusota rumande

Shamim, mumewe waendelea kusota rumande

08 July 2019 Monday 16:40
Shamim, mumewe waendelea kusota rumande

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

KESI ya uhujumu uchumi inayomkabili, mfanyabiashara, Abdul Nsembo maarufu Abdulkandida(45) na mkewe, Shamim Mwasha(41),inasuburi majibu ya kielelezo kutoka kwa mkemia mkuu wa serkali.

Wakili wa Serikali, Simon Wankyo amedai leo Julai 8,2019 mbeleya ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa kinachosubiriwa ni majibu ya kielelezo kutoka kwa mkemia mkuu wa serkali nakuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Wakili wa utetezi, Hajra Mungula alidai washtakiwa wako ndani na hawana dhama na kuutaka upande wa mashtaka kufwatilia kielelezo hicho ili majibu yapatikane kwa wakati.

Hakimu Mhina  baada ya kusikiliza maelezo ya hayo, aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 22, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande.

Shamimu ambaye ni mmiliki wa Blog 8020 Fashion na mumewe wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2019.

Washitakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Mei 13, mwaka huu.

Shamim na mumewe walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi ambayo ni kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70

Inadaiwa Mei Mosi, mwaka huu  wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini  Dar es Salaam, washitakiwa walisafirisha dawa hizo.

 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.